KESI ambazo
zinazowakabili watuhumiwa wanaowafanyia ukatili watoto wadogo mkoani Shinyanga,
zimedaiwa kukosa ushirikiano kwa upande wa mashahidi na kusababisha kesi hizo
kufutwa bila ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua yeyote ya kisheria.
Hayo
yamebainishwa jana na Afisa wa ulinzi wa usalama wa mtoto Hermani Mmbunda, kutoka
Shirika la Save the Children , linalofanya Shughuli zake mkoani Shinyanga,
amesema asilimia kubwa ya kesi zinazopelekwa mahakamani juu ya ukatili kwa
watoto wadogo zimekuwa hazifiki hadi mwisho kutokana na mashahidi kushindwa
kutoa ushirikiano wakutosha.
Mmbunda amesema Shirika
lao limekuwa likisaidia jamii inayotendewa vitendo hivyo, katika hatua ya awali
hadi ngazi ya mahakama, lakini linapofika suala la ushahidi wa mtu
aliyeshuhudia tendo hilo,wamekuwa hawahudhulii mahakani na wengine kukana
hawajui chochote juu ya tukio hilo.
‘’katika kesi
hizi za ukatili dhidi ya watoto, asilimia kubwa zimekuwa zikiisha kinyemela
kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha mahakani, ambapo mashahidi wa kesi
hizi,wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha na wengine wakikana shitaka hilo”
alisema Mmbunda na kuongeza kuwa.
“Tulipofanya
utafiti juu ya suala hili la Mashahidi kutohudhuria na kukana matukio hayo,tuka
baini kuwa asilimia kubwa ya watuhumiwa wa matukio hayo wanatoka ndani ya jamii
husika (Ukoo), ambapo wamekuwa wakiitishana vikao vyao na kumaliza suala hilo
kimyakimya na hivyo kupunguza nguvu ya kesi hiyo mahakamani”
Mmbunda alisema
baadhi ya Mashahidi hao wamekuwa wakidai kutishiwa kutengwa na ukoo, huku
wengine wakitishiwa maisha, na kuwafanya wakate tamaa ya kuendelea kutoa
ushahidi mahakani dhidi ya kesi hizo za ukatili.
Amesema kufuatia
matukio hayo Shrika hilo la Save the Children,limepanga mkakati kwa kushirikiana
na mashirika mengine yanayotetea haki za
mtoto mjini humo,ikiwamo na serikali,
katika kuhakikisha wanatoa elimu ndani ya jamii kuanzia ngazi ya kata,vitongoji
,vijiji hadi wilaya.
Naye afisa ustawi
wa jamii katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Nghabi, alisema katika matukio
100,ya ukatili dhidi ya watoto yaliyolipotiwa mwaka jana (2013), kesi zilizopelekwa
mahakamani na kutolewa ushahidi na watuhumiwa kufungwa jera ni kesi 27 tu kati
ya Miamoja.
Nghabi alisema,
kufuatia wananchi kushidwa kutoa ushahidi dhidi ya kesi hizo, huku wengine
wakiwaficha watuhumiwa kumeendelea kuchangia kuwepo kwa matukio ya kikatili dhidi ya watoto wadogo mkoani
humo.
|
0 Response to "MASHAHIDI KESI ZA UKATILI,UBAKAJI WAMEKUWA HAWAJITOKEZI MAHAKAMANI NA KUISHA KINYEMELA."
Post a Comment