Habari za hivi Punde

DIWANI WA CCM AKAMATWA AKIWA NA MATUNGURI YA DAWA AKIWATAPELI WATEJA WAKE..

Wakati serikali ikiendelea kupiga vita waganga wa kienyeji matapeli hali imekuwa tofauti huko Geita ambapo diwani wa CCM  Mawazo Wiliam  wa kata ya ya Bugarama  Wilayani Geita amekamatwa akiwa na matunguri anayoyatumia nyumbani kwake kupiga ramli chonganishi na kuosha wakataji wa mapanga .

Wakiongea kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi wa kata hiyo kwa sharti la kutotaka kutajwa majina yao  walisema diwani huyo amekuwa ni kero kwa watu kwani amekuwa akiwatapeli watu kwa kuwapatia tiba za uongo na kuwachonganisha watu bila kuona kuwa yeye ni kiongozi.

Walisema diwani huyo amekuwa akiwapigia ramli chonganishi watu wanaokwenda kwake kwa ajili ya kupata tiba ya kienyeji hivyo kuwaomba wanaohusika kuchukua hatua dhidi ya diwani huyo.
"Jamani huyu diwani wa CCM ni tapeli anawachonganisha wananchi mpaka wanafika hatua ya kuuana ,kwanza si mganga bali ni tapeli ni mganga gani ufike unaambiwa kiasi kikubwa cha fedha ",walisema.

Afisa mtendaji wa kata hiyo Juma Choba  alikiri kukamatwa kwa diwani wake  lakini akasema kuwa  alikamatwa kwa tuhuma za kuwaosha wakataji wa mapanga  katika kata hiyo.

Hata hivyo alisema hajui kama ni kweli anafanya kazi hiyo kwani hajawahi kuona ila anasikia kutoka kwa wananchi kuwa diwani wake anawapigia ramli chonganishi.

"Mimi nasikia kama wewe unavyosikia lakini sijawai kumuona ila amekamatwa yuko Polisi Wilayani inawezekana ni kweli kwa kweli siwezi kukataa",alisema Mtendaji huyo.

Akizungumza na malunde1 blog iliyotaka kujua zaidi kuhusu tuhuma hizo za kukamatwa kwake na kupiga ramli chonganishi , diwani Mawazo alisema kuwa yeye hana lolote la kujibu juu ya hilo.

Jeshi la polisi  Mkoani Geita limethibitisha kukamatwa kwa diwani Mawazo na uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geit

0 Response to "DIWANI WA CCM AKAMATWA AKIWA NA MATUNGURI YA DAWA AKIWATAPELI WATEJA WAKE.."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.