Kwa
mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma
Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi
kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo
walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa
imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.
“Mwili
wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha
hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi
kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu.
Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika.
Ijumaa
iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya
kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya Landcruiser.
Watu zaidi ya 40 walifariki na wengine 79 kujeruhiwa.
0 Response to "MTU ALIYEZIKWA AKIWA NA SIKU TATU KABURI LAKE LAFUKULIWA HUKO BUTIAMA."
Post a Comment