Habari za hivi Punde

POLISI USHIROMBO WABAINI SMG SABA,WAMSHIKILIA MMOJA AKIWA AMEBEBA BOMU JUU YA MTI

KATIKA  msako uliofanywa jana na jeshi la polisi nchini katika mkoa wa Geita  eneo la ushirombo wilaya ya Bukombe  wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja waliyekuwa wakimhisi kuwa ni jambazi  huku akiwa ameketi juu ya mti na kushikilia bomu.

Mtu huyo ambaye hakufahamika jina alikutwa juu ya mti majira ya jioni wakati msako mkali wa jeshi la polisi ukiendelea katika eneo hilo huku wakikuta bunduki saba aina ya SMG zikiwa zimewekwa kwenye tanuru la kuchomea matofali.

Ambapo jeshi hilo pia lilimkamata huku likimficha sura yake kwa kitambaa cheusi kwa kumhisi kushiriki kitendo cha kuua askari wawili   waliokuwa zamu katika kituo kidogo cha polisi na watatu kujeruhiwa huku taarifa zikieleza kuwa askari mmoja aliyekuwa majeruhi alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza.

Hata hivyo jeshi la polisi nchini limetangaza dau  la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo.

KARENY. Powered by Blogger.