Habari za hivi Punde

WAZIRI WA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI -DK MWAKYEMBE AAGIZA MAKAMPUNI YA MABASI YALIYOPATA AJALI KUFUNGIWA


Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya  J4 Express  na  Mwanza Coach yafungiwe mara moja..

Dk Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39  na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.

“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha sana. 

Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.

Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi. 

“Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.

Na Elvna Stambuli

KARENY. Powered by Blogger.