Katika
kuendeleza habari za uchunguzi nchini Mfuko wa vyombo vya habari (TMF)
umetoa ruzuku ya Sh. bilion 1.7 kwa vyombo vya habari 16.
Mkurugenzi
wa TMF, Ernest Sungura, alisema jana wakati wa kutia saini mkataba wa
mwisho wa kutekeleza makubaliano ya kufanya habari za uchunguzi nchini.
Sungura
alisema ruzuku hiyo inatakiwa kutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa na
kwamba wamewaweka wakaguzi wao wa ndani watakaokagua mara kwa mara.
“Ruzuku hiyo
imetokana na msaada wa kodi za wananchi kutoka nchi za Denmark,
Swissland, Norway na Uingereza kwa ajili ya kutatua matatizo yaliyopo
hivyo inatakiwa kuzithamini na kuweka nidhamu kubwa,” alisema.
Sungura
alisema, kwa atakaye fuja au kutumia vibaya ruzuku hiyo atakuwa
anajitafutia ubaya na kwamba hatapata tena nafasi ya kupata ruzuku hiyo
ambayo hutolewa kila mwaka.
Aidha,
alisema jamii ipo katika changamoto kadhaa hali ambayo inasababisha
maisha ya watu kutobadilika, vyombo vya habari vinatakiwa kuliangalia
suala hilo katika kuibua mambo mbalimbali ili kuwepo na mabadiliko.
Alisema
mahitaji muhimu ya binadamu hayapatikani katika jamii ikiwamo huduma za
afya, shule na vitu vingine vya muhimu vimekuwa havipatikani kutokana na
changamoto za tabia za kibadhirifu.
Aliongeza
kuwa vyombo vya habari vinahesabiwa kuwa ni muhimili ambao siyo rasmi
wakati ni muhimili muhimu unaofanya kazi kubwa na kuibua mambo
mbalimbali yakiwamo ya ufisadi.
Aidha,
alisema mkakati wao ni kuendelea kuviwezesha vyombo vya habari katika
kuibua maovu ndani ya jamii, ili changamoto hizo ziweze kufanyiwa kazi.
Ruzuku hiyo
imegawanywa katika makundi mbalimbali na kwamba chombo cha habari
kilichopata ruzuku kubwa ni Sh. milioni 185 na cha mwisho kimepata Sh.
milioni 50.
Na Beatrice Shayo.
0 Response to "TMF YATOA JUMLA YA SHILINGI BILLIONI 1.7 KWENYE VYOMBA MBALIMBALI VYA HABARI CHINI."
Post a Comment