|
MKURUGENZI
Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama;Felix Kimario akitoa neno
wakati wa makabidhiano ya vitanda 27 vya Wagonjwa vilivyotolewa katika
Hospitali ya wilaya ya Kahama,chini ya Ufadhili wa Mgodi wa Dhahabu wa
Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine.
MKUU
wa Wilaya ya KahamaBenson Mpesya amewataka watumishi katika hospitali ya
Halmashauri ya mji wa Kahama kufanya kazi kwa weledi bila kujali mgawanyo wa
kiutawala uliofanywa wakati wa kuigawa wilaya hiyo.
Kauli
hiyo ameitoa leo mjini Kahama wakati akipokea msaada wa vitanda 27 vya kisasa
vya wagonjwa katika hospitali hiyo vilivyotolewa na Kampuni ya African Barrick
Gold Mine kupitia Mgodi wake wa Buzwagi.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
MKUU
wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza na Waganga,Wauguzi na
baadhi ya watu mbele ya mojawapo ya Vitanda 27 ambacho kilikuwa
kimelaliwa na mmoja wa Wasanii wa KMCT,wengine katika picha ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Felix Kimario{Mwenye
suti},Mwenye miwani na kofia ni Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa
Buzwagi;George Mkanza,Kushoto kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Mji ni Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Kahama;Dk.Deo Nyaga na aliyenyuma ya
Mkuu wa wilaya aliyeshika kipaza sauti ni Muuguzi Shaabani Abdallah.
Katika makabidhiano hayo Mpesya amesema ameshangazwa na
mgawanyo wa kiutawala wa wilaya ya Kahama iliyogawanywa kwenye halmashauri tatu
za Mji,Ushetu na Msalala mgawo huo umeathiri huduma za afya.
Aidha
Mpesya amesema mgawo huo pia umekwenda sambamba na hospitali ya wilaya ambayo
nayo imegawanywa katika Halmashauri tatu hali liyodhoofisha utendaji kazi kwa
kuwagawa madaktari katika halmashauri tatu,badala ya kuimarisha moja ya
wilaya.
| |
|
|
Alipendekeza Madiwani hao wangeweza kutumia busara wakaacha
kuigawa hospitali hiyo ambayo imesimama kama ya Rufaa kwa kutoa huduma kwa
wagonjwa wanaotoka katika Halmashauri zao,badala ya kuwapeleka Madaktari kwenye
zahanati za vijiji,huku wilaya kukiwa na mapungufu.
Naye
Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanza amesema vitanda hivyo
vimetolewa na Madaktari rafiki wa Kampuni hiyo toka nchini Austaria na
vimegharimu Shilingi Milioni 54.
0 Response to "MGODI WA DHAHABU BUZWAGI WAFADHILI VITANDA VYA WAGONJWA HOSPITALI YA WILAYA KAHAMA."
Post a Comment