Habari za hivi Punde

WANANCHI WA MKOANI GEITA WASHITUSHWA KWA KUKITHIRI KWA MATUKIO


Wananchi wilayani Geita Mkoani Geita wamemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Ernest Mangu(PICHANI) kumrudisha aliyekuwa kamanda wa wa mkoa huo Leonad Paulo aliyehamishiwa mkoa wa Morogoro hivi karibuni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoa huo wametoa kilio hicho kutokana na kukithiri kwa mauaji yanayosababishwa na majambazi ambao wamefanya wakazi wa mji huo kukosa amani na kushindwa kufanya kazi zao za kila siku kwa kuogopa kuvamiwa.

Wamesema katika kipindi yupo kamanda Paulo majambazi waliisha na mauaji ya vikongwe yalipungua kwa kasi lakini kwa sasa vikongwe wanazidi kukatwa na kuuawa huku majambazi wakizidi kumaliza maisha ya ndugu na jamaa na sasa wameanza kuua askari polisi.

Wamesema matukio makubwa ambayo yametokea kwa kipindi cha  muda mfupi tangu kamanda Paulo aondoke ni lile la majambazi kuwavamia wafanya bishara wawili na kumuua mmoja wao Gozibati Warwa aliyeuawa mchana kweupe saa kumi na moja jioni  na kuchukua pesa na bastola na kutokomea na kukamatwa mda mfupi.

Mmoja wa mwananchi hao Masanja Juma kutoka Katoro wilayani Geita amelitaja tukio la pili kuwa ni  lile la majmbazi  kuvamia kituo cha polisi  cha Bukombe na kuua askari wawili ambao ni PC Dastan Kimati(25) na Horia Mwandija(30)  na kujeruwi wawili, Mohamed Hassan(25 na Devid Ngutama(44) ambapo pia walibeba bunduki na mabomu pamoja na risasi na kutokomea kusikojulina

Amesema  japokuwa  bunduki inasemekana zimekamatwa lakini wananchi bado wana hofu kubwa.
"Mimi kama mwananchi wa Geita namuomba (IGP) amrudishe Kamanda Paulo kwani alikuwa anajaribu kutumia mda mwingi kuongea na watu wa aina zote,ofisi yake ilikuwa wazi kila wakati  kwa watu wote, ndio maana na alipopelekewa tatizo alifuatilia mara moja na kutatua" amesema Juma.
Hata hivyo kufuatia matukio ya kuendelea kuuawa kwa watu yamezidi kuwafanya wakazi wa mji huo kutofanya kazi zo kwa uhuru hivyo wamemwomba IGP kutenga kanda maalumu katika mkoa wa Geita huenda ikapunguza mauaji.

0 Response to "WANANCHI WA MKOANI GEITA WASHITUSHWA KWA KUKITHIRI KWA MATUKIO "

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.