AKIENDA HARUSINI BAADA YA BOTI YAO KUSOMBWA NA MAJI AKIWEMO BWANA HARUSI
Takriban
watu 17 akiwemo bwana harusi na watoto wawili wamekufa maji baada ya
boti ya
uokoaji iliyokuwa imewabeba wageni kwenda kwa sherehe ya harusi
kuzama katika mafuriko nchini Pakistan.Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2 nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa.
Maafisa wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan kufikia sasa.
Zahid Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao.
Maafisa wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko nchini Pakistan.
Msemaji wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la Punjab amesema kuwa familia hiyo ilionywa kuhusu mafuriko hayo.
Bi harusi amesema kuwa alinusurika baada ya kushika mti wa stima.
Mazishi ya waathiriwa 17 yamefanyika huku waokoaji wakiendelea kuwatufuta wale waliotoweka.
BBC.
0 Response to "WATU 17 AKIWEMO BIBI HARUSI WAMEFARIKI KUTOKANA NA AJALI YA BOTI ILIYOWABEBA."
Post a Comment