Habari za hivi Punde

NGASSA MCHEZAJI BALAA;MATAJI YAMIMINIKA AFANYA KUFURU;



Mfalme wa mataji; Mrisho akiwa na Ngao ya Jamii jana Uwanja wa Taifa, ambalo idadi ya mataji tisa aliyoshinda tangu aanze soka ya ushindani

MSHAMBULIAJI Mrisho Khalfan Ngassa jana ameshinda taji la tisa tangu aanze kucheza soka ya ushindani, kufuatia kuiongoza Yanga SC kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Ngassa jana ametimiza jumla ya mataji matano aliyowahi kushinda na Yanga SC katika awamu mbili alizochezea klabu hiyo.
Ngassa alijiunga na Yanga SC mwaka 2007 na kabla hajahamia Azam FC alishinda mataji matatu Jangwani, ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili na Kombe la Tusker mara moja.

Hongera kijana; Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad akimpongeza Mrisho Ngassa jana

MATAJI ALIYOWAHI KUSHINDA MRISHO NGASSA

2006 Tusker Kagera Sugar
2008 Ligi Kuu Yanga SC
2009 Ligi Kuu Yanga SC
2009 Tusker Yanga SC
2010 Challenge Kili Stars
2011 Mapinduzi Azam FC
2012: Ngao        Simba SC
2013 Ngao  Yanga SC
2014 Ngao Yanga SC
Wakati anaingia Yanga SC Ngassa alikuwa ameshinda taji moja tu, Kombe la Tusker akiwa na Kagera Sugar.
Na alipokwenda Azam FC mwaka 2010, Ngassa pamoja na kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, pia alishinda Kombe la Mapinduzi na klabu hiyo.    
Alipohamia Simba SC nako akashinda Ngao ya Jamii katika msimu mmoja wa kuitumikia na baada ya kurejea Yanga SC, ametwaa Ngao mara mbili mfululizo.
Hata hivyo, mwaka jana Ngassa alijiunga na wenzake kusherehekea ushindi wa Ngao kwa kuifunga Azam tena 1-0 akitokea jukwaani, kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu. 
Ngassa ambaye kwa sasa anaongoza kwa mabao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ingawa Yanga ilikwishatolewa mapema, pia amewahi kushinda Kombe la Challenge akiwa na Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.

0 Response to "NGASSA MCHEZAJI BALAA;MATAJI YAMIMINIKA AFANYA KUFURU;"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.