Habari za hivi Punde

KATIBU WA CCM TAIFA KINANA; APANDISHA MILIMA YA USAMBARA KWA KUENDESHA BAISKELI KWENDA JIMBO LA MKINGA MKOANI TANGA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg'aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga,  mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.
Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiongoza msafara katika safu ya milima ya Usambara kwenda Jimbo la Mkinga, Tanga.
Ni safari ndefu lakini yenye faraja na matumaini
Mbele ni Kinana na Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Uhuru, Seleman Jongo
Kinana mbele na kutoka kushoto ni wanahabari walio kwenye msafara huo, David John wa Majira, Seleman Jongo wa Uhuru na Said Mwishehe wa Jambo leo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga.
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama baada ya kutumia usafiri wa baiskeli

Wanahabari waliosafiri kwa baiskeli wakipumzika baada ya kufika katika Kata ya Mg'aro
Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg'aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga
Watoto wakiwa juu ya kisiki cha mti wakiwa na hamu ya kumuona Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia katika Kata ya Mg'aro.
Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mg'aro ambapo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mkinga itaboreshwa, halafu na umeme utawekwa katika Kata hiyo.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya msafara wake kukabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mkinga katika Kata ya Daluni.
Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Maramba.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Polisi Maramba
Wananchi wakishangilia baada ya msafara wa Kinana kuwasili katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Duga, Uwanja wa Maforoni, wakati wa ziara yake wilayani Mkinga.
Wananchi wakishangilia huku mmoja wapo akiwa na bango la kuisifia CCM katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni,  Kata ya Duga.
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji
Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga.
KARENY. Powered by Blogger.