Habari za hivi Punde

MTUHUMIWA ALIYEWEKWA MAHABUSU INYALA -MBEYA AMEKUTWA AMEJINYONGA

 
Mahabusu aitwae Andaluswe Mwakapila mkazi wa Olongo Mbeya amejinyonga na kufariki dunia akiwa ndani ya mahabusu katika kituo kidogo cha Polisi Inyala ambapo Kamanda wa Polisi  Mbeya Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema mwili wa marehemu ulikutwa unaning’inia katika dirisha la chumba cha mahabusu.
Alijinyonga kwa kutumia shati lake ambapo chanzo cha kujiua inasemekana kabla ya kufikishwa mahabusu  alikua na ugomvi na mkewe ambapo alimpiga kwa kutumia shoka na jembe na kumsababishia majeraha mengi
KARENY. Powered by Blogger.