UMILIKI WA ARDHI CHANZO CHA KUTONUFAISHA WAJASIRIAMALI
MENEJA wa Azania Tawi la Kahama,Godfrey Mahona akiongea. |
IMEDAIWA kuwa tatizo la umiliki wa
ardhi katika maeneo yasiyo pimwa na mpango miji yakiwemo ya vijijini ni sababu
inayokwamisha wajasiliamali wengi kukosa fursa ya kupata mikopo
mikubwa kutoka
kwenye vyombo vya fedha
Hayo
yalibainishwa na Meneja wa benki ya Azania tawi la Kahama Godfrey Mahona wakati
akitoa maada ya mafunzo ya ujasiliamali kwa wafanyabiashara wa kata ya
Bulyanhulu wilayani Kahama yaliyofanyika kwenye kijiji cha Kakola Halmashauri
ya Msalala
Meneaja
huyo alisema tatizo hilo la kutopimwa kwa maeneo ya ardhi ya vijijini
imechangia kwa kiwango kikubwa kuwakosesha umiliki wa kudumu na hivyo kuwa
chanzo cha baadhi ya wajasiliamali kuambulia wasitani wa mkopo wa Shilingi Milioni
kumi badala ya kupata fedha zaidi ya Milioni 50
Awali
mwenyekiti wa wajasilamali hao Robert Zungu aliwaomba wafanyabiashara wenzake kutumia fursa ya
mafunzo hayo yanayotolewa na Benki ya Azania ambayo yatawasaidia kupata elimu
ya kuweza kukopa na kurejesha kwa muda kuwa chachu ya kukomboka kimtaji na
kupiga hatua za kiuchumi kupitia miradi yao.
Kufuatia
hali hiyo Mahona alisema upo umuhimu wa Benki yake kuwasaidia
wajasiliamali hao kupimiwa maeneo yao ambapo halmashauri ya wilaya husika
inaweza kuingia mkataba na taasisi yake juu ya ulejeshwaji wa gharama za kupimiwa
ambapo kila mwananchi mwenye mahitaji hayo anaweza kuchangia
0 Response to "UMILIKI WA ARDHI CHANZO CHA KUTONUFAISHA WAJASILIAMALI."
Post a Comment