HATIMAYE
baada ya kuibuka uvumi siku ya Jumanne kuamkia Jumatano juu ya kufariki kwa
rais wa Zambia Michael Sata, Serikali ya nchi hiyo imethibitisha kifo chake.
Kwa mujibu wa katibu wa
baraza la mawaziri, Roland Msiska amethibitisha kifo hicho cha Sata {77} kilichotokea baada ya rasi huyo kusafirii
kuelekea jijini London Uingereza juma moja lililopita kwaajii ya kupata
matibabu.
Akitoa tangazo hilo
alfajiri, Roland aliwaambia wananchi wa Zambia kwa masikitiko makubwa angependa
kutangaza kifo cha rais wao aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Uingereza.
Tangazo hili
linathibitisha madai ya vyama vya upinzani na watu wa karibu wa rais Sata ambao
mara kadhaa walidai kuwa kiongozi huyo anaugua na ameshindwa kutekeleza
majukumu yake kama rais lakini mara zote Serikali imekuwa ikikanusha hadi juma
moja lililopita ilipothibitisha kuugua kwa rais Sata.
Wakati alipokuwa akiondoka
kuelekea jijini London kwa matibabu, rais Sata alimteua waziri wa ulinzi na
sheria Edgar Lungu kukaimu madaraka ya rais kwa kipindi ambacho hatokuwepo.
Makamu wa rais Guy Scott
ambaye mara kadhaa amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za Serikali kama
kiongozi wa nchi, yeye ana uraia wa Uskochi hali ambayo inamfanya ashindwe kuwa
rais kamili wa taifa la Zambia kwakuwa wazazi wake hawakuzaliwa nchini Zambia.
Sata ambaye alibatizwa
jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa mwaka
2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa
wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzania.
Hivi karibuni rais Sata
alianza operesheni dhidi ya wapinzani wake na waandishi wa habari wlaiokuwa
wakikosoa Serikali yake jambo ambalo lilianza kumchora kama mmoja wa viongozi wababe
kusini mwa bara la Afrika.
0 Response to "RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIA "
Post a Comment