Habari za hivi Punde

MKAZI WA KIJIJI CHA MWAKITOLYO WILAYANI SHINYANGA AVAMIWA USIKU NA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE.

Mkazi wa kijiji na kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga  Mageni Buhimili(54)  ameuawa kwa kukatwa panga kichwani,mikononi na tumboni wakati akila chakula cha usiku nyumbani kwake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Oktoba 26 mwaka huu saa moja na nusu usiku.Kamanda Kamugisha  alisema  mkazi wa kitongoji cha Mahiga kata hiyo akiwa anakula chakula cha usiku ghafla alivamiwa na watu wasiojulikana kisha kumuua kwa kumkata panga kichwani,mikononi na tumboni.


Alisema juhudi za kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hilo zinaendelea.


Wakati huo huo jeshi la polisi linawashikilia watu watatu wakazi wa kata ya Idahina wilayani Kahama kwa kosa la kukutwa wakimiliki silaha aina ya bastola na gobole kinyume cha sheria.

Kamanda Kamugisha alisema watu hao walikamatwa Oktoba 27 mwaka huu.


Aliwataja watu hao kuwa ni Magashi Magunga(21) mkazi wa Chato mkoa wa Geita na Masumbuko Juma(27) mkazi Ushirombo ambao walikamatwa kwa kupatikana na silaha aina ya bastola.


Alisema silaha hiyo imetengenezwa kienyeji isiyokuwa na namba za usajili wakimiliki kinyume cha sheria na kwamba wanahojiwa ili kubaini matukio ya kihalifu waliyokuwa wakiyafanya.

KARENY. Powered by Blogger.