Hapa
ni katika kijiji cha Mwabomba (mnadani) kata ya Idahina halmashauri ya
Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako leo mwenge wa uhuru
umepokelewa na katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo ukitoka
Geita.Katibu tawala mkoa wa Geita Severine Kahitwa amekabidhi kwa
katibu tawala mkoa wa Shinyanga ambaye naye kakabidhi kwa mkuu wa wilaya
ya Kahama Benson Mpesya .Mwenge huo leo upo Ushetu,kesho mji Kahama
kesho kutwa Msalala. Ukiwa Shinyanga jumla ya miradi 58 yenye thamani ya
shilingi bilioni 7.6 itazinduliwa-Picha zote na Kadama Malunde
Huyu ni mtu_ Moja
ya kati ya burudani zilizokuwepo wakati wa mapokezi ya mbio za mwenge
wilayani Kahama leo,ambapo mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri 6
za mkoa wa Shinyanga yaani Ushetu,Kahama mji,Msalala,Shinyanga,manispaa
ya Shinyanga na Kishapu sawa na kilomita 1188
|
Mcheza ngoma ya Mashanga kutoka kijiji cha Nundu kata ya Chela halmashauri ya Ushetu akifanya yake |
|
Ngoma ya Wagoyangi,jamaa anacheza na nyoka |
|
Eneo la mapokezi ya Mwenge wa uhuru leo Shinyanga |
|
Viongozi mbalimbali wa mkoa w Shinyanga wakijiandaa kupokea mwenge wa uhuru leo |
|
Wanafunzi walijitokeza kwa wingi |
|
Tunasubiri Mwenge...... |
|
Burudani inaendelea,akina mama kutoka Kahama wakifanya yao |
|
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwabomba wakicheza viduku |
|
Mama huyu mjamzito uvumilivu ulishinda akajitokeza kucheza wimbo wa Bhudagala" Kundi Wa Ng'wamoto" |
|
Shamra shamra za mwenge wakazi wa Mwabomba walijitokeza kwa wingi,wengine wakapanda juu ya miti |
|
Kutoka Geita-Mwenge Unaletwa Shinyanga |
|
Mwenge unawasili Mwabomba |
Mwenge uko Mwabomba
Mwenge ukiwa eneo la mapokezi Mwabomba Kahama
Shamra shamra za mwenge zinaendelea
|
Katibu tawala mkoa wa Geita Severine Kahitwa akisoma taarifa kabla ya kukabidhi mwenge mkoa wa Shinyanga |
0 Response to "VITUKO VIMETAWALA MWENGE WA UHURU MKOANI SHINYANGA ANGALIA PICHA ZAIDI"
Post a Comment