Habari za hivi Punde

PSI ;IMENYANYUA VIPAJI VYA SOKA KWA VIJANA MKOANI TANGA KWA KUDHAMINI MASHINDANO YA MALARIA CUP

MASHINDANO ya  Malaria Cup yanayoletwa  kwenu na PSI Ofisi ya mkoa wa Tanga kupitia  ofisi ya Wakati sports Promoters  ambapo lengo lake limeelezwa na  mratibu wa mawasiliano  kanda ya Kaskazini  Victor  Mapile  kuwa mashindano hayo ni kuhamasisha  wananchi wa mkoa  wa Tanga  pamoja na wilaya zake kujikinga dhidi ya  ugonjwa wa malaria ,hivyo wananchi wanahimizwa  kulala katika vyandarua  vilivyowekwa dawa kila siku,pia wakumbuke  ugonjwa wa malaria unaua  hasa kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano na kushauriwa wananchi kwenda kupima mara wanapojisikia  dalili za homa  kwasababu sio kila homa ni malaria"tushirikiane kuitokomeza malaria haikubaliki"

Wakwanza kushoto ni diwani viti maalumu kutoka Handeni Monica  Msagusa aliyeketi kati ni meneja wa PSI  kutoka mkoani Tanga  Geofrey Mwankenja  na pembeni yake kulia ambaye  alikuwa mgeni rasmi  kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga  Clement  Marcela wakiwa wameketi meza kuu tayari kusubiri ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Malaria CUP.

Meneja wa PSI mkoa wa Tanga Mwankenja  akiwa na kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga  Marcela akisubiri kukaribishwa katika ufunguzi wa  Malaria Cup.

Meneja kutoka ofisi ya wakati sports promoters Fredrick  Sospeter   akiwa na mkurugenzi wa ofisi hiyo Sophia wakati wakisubiri ufunguzi wa mashindano hayo ya mpira wa miguu yatakayo shirikisha timu 49  kutoka katika wilaya sita za mkoa wa Tanga ambapo mchezo  wa mashindano ya malaria cup ikiwa kwa wilaya ya  Tanga timu nane zinashiriki  uwanja wa gofu juu majani mapana.

Timu ya watoto iliyoshiriki katika kuburudisha mashabiki  kutoka gofu juu majani mapana wakati wakijiandaa kuingia uwanjani.

Mkurungezi wa ofisi ya wakati sports promoters  mkoani Tanga Sophia Wakati akiwa na  mratibu wa mawasiliano  kanda ya kaskazini Victor  Mapile  wakiangalia ratiba ya mashindano hayo yanavyokwenda.

Hapa ilifika wasaa wa meneja wa kutoka ofisi ya  wakati sports promoter  Sospeter akieleza kuhusu mashindano hayo  na kuwashauri jamii kuzingatia ujumbe uliotolewa dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa Malaria.

Mkuu wa kituo cha polisi Chumbageni Omary Mtundu akisalimia na mgeni rasmi kaimu mganga mkuu wa mkoa Marcela  baada ya kuwasili meza kuu.

Timu ya watoto iliyoandaliwa kutoa burudani kabla ya mashindano  rasmi kuanza.

Walioshiriki kutazama mashindano ya Malaria Cup yaliyoandaliwa na  Wakati sports Promoter na kudhaminiwa na PSI mkoani Tanga.

Wafanyakazi wa  REDCROSS  kutoka mkoani Tanga baada ya kuwasili katika uwanja wa gofu juu majani Mapana tayari  kujiandaa kwa kuanza kutoka huduma ya kwanza kwa mwanamichezo yoyote atakaye umia akiwa uwanjani.



Timu za watotoiliyovaa jezi rangi ya njano ni  kutoka timu ya Kagera FC  yenye makazi yake majani Mapana  na timu iliyovaa jezi rangi nyekundu ni timu kutoka  kata ya Majengo  zote za wilayani Tanga.


Hizi ni timu zilizoshiriki katika mashindano ya Malaria Cup ambapo Timu iliyovaa jezi Nyekundu ni kutoka Majengo Fc ambayo katika mchezo huo baada ya kufunguliwa rasmi walicheza na timu ya Kagera FC kutoka majani Mapana na kufanikiwa kushinda goli nne kwa bila .

0 Response to "PSI ;IMENYANYUA VIPAJI VYA SOKA KWA VIJANA MKOANI TANGA KWA KUDHAMINI MASHINDANO YA MALARIA CUP"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.