Habari za hivi Punde

AMUUA MWANAYE KWA KOSA LA KUMUNYIMA PESA YA KUNUNULIA POMBE.

NA. AHMEID ABDULAZIZ, NACHINGWEA

Katika tukio la kwanza Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Binasa Saidi(66) mkazi wa kijiji cha Kipara kata ya Mnero aliuwawa kwa kupigwa na kipande cha mti kichwani. Katika tukio hilo lililotokea saa 3 usiku katika kijiji hicho, Binasa aliuwawa na mwanawe wa kumzaa anayetambulika kwa jina la Mohamedi Chigololo(37) baada ya kutokea mabishano baina yao.


Taarifa zilizopatikana kutoka kijijini hapo na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Zimeeleza kuwa Chigogolo ambaye ni fundi uashi alimuuwa mama yake mzazi huyo kutokana na kuchukizwa na kitendo cha mama yake kutompa fedha ili akanywee pombe. Ambapo baada ya kumuomba na kujibiwa kuwa hakuwa na fedha alimshikia gongo lamti na kuanza kumfukuza na kufanikiwa kumkuta na kumpiga kichwani na kusababisha mama huyo kupoteza fahamu na kufa baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mnero. 
Chigololo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya mauaji hayo, baada ya wananchi wa kijiji hicho kumkamata alipojaribu kukimbia. Ambapo baada ya kumkamata walimfikisha kwenye ofisi ya serikali ya kijiji hicho.
Katika tukio la pili Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Getrude Yusufu(25) mkazi wa Kilimanihewa mjini Nachingwea, alikutwa ananing'inia juu ya mwembe akiwa kajinyonga kwa kutumia shuka.

Tukio hilo ambalo pia limethibitishwa na kamanda Mzinga imeelezwa kuwa Getrude alikutwa alfaji ya usiku wa tarehe 2 mwezi huu akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka katika kijiji cha Matangini kata ya Nangowe, wilayani Nachingwea. 

Ambapo mwili wake ulikutwa unang'inia juu ya mwembe jirani na mashine ya kusaga nafaka inayomilikiwa na askari wa jeshi la polisi anayetambulika kwa jina la Siku Athumani ambaye ndiye aliyeiona maiti hiyo wakati anakwenda kuangalia mashine yake. Sababu za mwanamke huyo kujinyonga hazikuweza kufahamika kutokana kutoacha maandishi yenye maelezo.
KARENY. Powered by Blogger.