Habari za hivi Punde

PSI; YAJIZATITI KUTUMIA VIJANA KATIKA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KUPINGA UGONJWA WA MALARIA MKOANI TANGA.


Zawadi zilizoandaliwa  kwa washindi walioshiriki  ligi ya  Malaria Cup iliyoandaliwa na PSI.

MASHINDANO ya  Malaria Cup yanayoletwa  kwenu na PSI Ofisi ya mkoa wa Tanga kupitia  ofisi ya Wakati sports Promoters  ambapo lengo lake limeelezwa na  mratibu wa mawasiliano  kanda ya Kaskazini  Victor  Mapile  kuwa mashindano hayo ni kuhamasisha  wananchi wa mkoa  wa Tanga  pamoja na wilaya zake kujikinga dhidi ya  ugonjwa wa malaria ,hivyo wananchi wanahimizwa  kulala katika vyandarua  vilivyowekwa dawa kila siku,pia wakumbuke  ugonjwa wa malaria unaua  hasa kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano na kushauriwa wananchi kwenda kupima mara wanapojisikia  dalili za homa  kwasababu sio kila homa ni malaria"tushirikiane kuitokomeza malaria haikubaliki"


Wakwanza kushoto ni diwani viti maalumu kutoka Handeni Monica  Msagusa aliyeketi kati ni meneja wa PSI  kutoka mkoani Tanga  Geofrey Mwankenja  na pembeni yake kulia ambaye  alikuwa mgeni rasmi  kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga  Clement  Marcela wakiwa wameketi meza kuu tayari kusubiri ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Malaria CUP.


Meneja wa PSI mkoa wa Tanga Mwankenja  akiwa na kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga  Marcela akisubiri kukaribishwa katika ufunguzi wa  Malaria Cup.


Meneja kutoka ofisi ya wakati sports promoters Fredrick  Sospeter   akiwa na mkurugenzi wa ofisi hiyo Sophia wakati wakisubiri ufunguzi wa mashindano hayo ya mpira wa miguu yatakayo shirikisha timu 49  kutoka katika wilaya sita za mkoa wa Tanga ambapo mchezo  wa mashindano ya malaria cup ikiwa kwa wilaya ya  Tanga timu nane zinashiriki  uwanja wa gofu juu majani mapana.


Timu ya watoto iliyoshiriki katika kuburudisha mashabiki  kutoka gofu juu majani mapana wakati wakijiandaa kuingia uwanjani.


Mkurungezi wa ofisi ya wakati sports promoters  mkoani Tanga Sophia Wakati akiwa na  mratibu wa mawasiliano  kanda ya kaskazini Victor  Mapile  wakiangalia ratiba ya mashindano hayo yanavyokwenda.


Hapa ilifika wasaa wa meneja wa kutoka ofisi ya  wakati sports promoter  Sospeter akieleza kuhusu mashindano hayo  na kuwashauri jamii kuzingatia ujumbe uliotolewa dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa Malaria.


Mkuu wa kituo cha polisi Chumbageni Omary Mtundu akisalimia na mgeni rasmi kaimu mganga mkuu wa mkoa Marcela  baada ya kuwasili meza kuu.


Timu ya watoto iliyoandaliwa kutoa burudani kabla ya mashindano  rasmi kuanza.


Walioshiriki kutazama mashindano ya Malaria Cup yaliyoandaliwa na  Wakati sports Promoter na kudhaminiwa na PSI mkoani Tanga.


Wafanyakazi wa  REDCROSS  kutoka mkoani Tanga baada ya kuwasili katika uwanja wa gofu juu majani Mapana tayari  kujiandaa kwa kuanza kutoka huduma ya kwanza kwa mwanamichezo yoyote atakaye umia akiwa uwanjani.
Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa kando ya uwanja na kushuhudia mechi iliyokuwa ikicheza atua ya mtoano katika viwanja vya gofu juu majani mapana ambapo timu ya Majengo Fc  ilinyukana na timu ya Kagera FC zote kutoka wilayani Tanga.




Mgeni rasmi Clement  Marcela ambaye ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga akifungua mashindano hayo huku akiwataka wananchi kujikinga dhidi ya ugonjwa wa malaria na kila homa sio malaria hivyo wajitahidi kupima afya zao na kujikinga pia kwani malaria haikubaliki ikiwa mkoa wa Tanga kwa wastani walio wengi hawana maambukizi ya ugonjwa wa Malaria bali wanapatwa na homa kutokana na maradhi mengine  waendelee kujikinga zaidi kwa watoto waliochini ya miaka mitano na mama wajawazito kwa kutumia pia vyandarua.

Mkurugenzi wa wakati sports promoters Sophia Wakati akitambulisha zawadi zilizpo mbele ya mgeni rasmi huku akieleza kuwa kila timu itakayoshiriki itapata zawadi ya jezi pamoja na mpira.

Zawadi zilizoandaliwa  kwa washindi walioshiriki  ligi ya  Malaria Cup iliyoandaliwa na PSI.
Kiongozi wa timu ya Vascodagama  akipokea zawadi ya jezi baada ya timu yake kushiriki ligi hiyo.
Mgeni rasmi Dkt  Clement akikabidhi zawadi hizo  kwa viongozi wa  ofisi ya Sophia Promoters.
Kiongozi wa timu akikabidhiwa zawadi na  mkurugenzi wa wakati sports promoters Sophia Wakati.

Zawadi ziwa tayari mezani.

zawadi

Timu za watotoiliyovaa jezi rangi ya njano ni  kutoka timu ya Kagera FC  yenye makazi yake majani Mapana  na timu iliyovaa jezi rangi nyekundu ni timu kutoka  kata ya Majengo  zote za wilayani Tanga.
Timu  ya  watoto kutoka Majengo ikijiandaa kuingia uwanjani.









PSI ;IMEJITOKEZA KUPINGA UGONJWA MALARIA KWA KUPITIA MICHEZO KWA VIJANA MKOANI TANGA,TAZAMA PICHA HAPA.

0 Response to "PSI; YAJIZATITI KUTUMIA VIJANA KATIKA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KUPINGA UGONJWA WA MALARIA MKOANI TANGA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.