Habari za hivi Punde

WANANCHI WA KATA YA KERENGE-KOROGWE WAPATA MASHINDANO YA MALARIA CUP

Mwenyekiti wa kamati ya huduma ya jamii halmashauri ya wilaya ya Korogwe vijijini  Shebila Iddi  akifungua mashindano ya Malaria Cup  katika kata ya Kerenge  wilayani humo yaliyodaminiwa na PSI mkoa wa Tanga na kuratibiwa na ofisi ya Wakati Sports Promoter ikiwa timu nane katika  kata hiyo zitashiriki ambapo ufunguzi wa kuanza kwa mashindano hayo yalifanyika kwenye uwanja wa  kerenge makaburini kati ya timu ya Moran FC  na Sato Fc.

Hii ni timu ya Sato FC ikiwa katika kujiandaa  kwa pambano  kwenye uwanja wa makaburini Kerenge hivyo mchezo huo ulikuwa mkali mpaka mwisho wa mchezo walitoka kwa goli mbili kila timu na baada ya hapo ilifuata hatua ya penati na kupigwa magoli  4-3 ikawalazimu kuaga mashindano hayo.


Mkurugenzi wa ofisi ya Wakati Sports Promoter iliyopo jijini Tanga  Sophia Wakati akiwaelezea  mashabiki  ambao hawapo pichani pamoja na wanamichezo waliohudhuria mchezo  huo wa ufunguzi  ambapo alisema lengo la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni  kunyanyua vipaji kwa vijana na kupinga ugonjwa wa malaria  kama inavyoeleza kauli mbiu malaria haikubaliki na kuwataka wananchi kutumia vyandarua na kwenda kupima afya zao.

Mwenyekiti wa kamati ya huduma ya jamii katika halmashauri  akijiandaa kukabidhiwa zawadi za timu shiriki wa mashindano ya Malaria Cup .

picha hii mwenyekiti wa huduma ya jamii ambaye alikuwa mgeni rasmi  baada ya kukabidhiwa zawadi za timu shiriki  akimkabidhi  kaimu mtendaji wa kijiji cha  Kerenge   Hassan  Makorongo.

Baadhi ya mashabiki na wachezaji  wakimsikiliza mratibu wa mashidano hayo  ambaye pia ni mkurugenzi wa Wakati Sophia Promoter Sophia Wakati katika uwanja wa  Kerenge Makaburini  uliopo  wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Mratibu wa mashidano ya Malaria  Cup yaliyodhaminiwa na PSI  Tanzania mkoani Tanga   akimkabidhi zawadi za jezi na mipira kwa mwenyekiti   Iddi  Sebila ambaye alikuwa mgeni rasmi

Hapa Sophia Wakati akionyesha  moja ya tisheti  ya jezi zinazotolewa kwenye mashindano hayo zilizotolewa na PSI na kubeba ujumbe  wa Malaria haikubaliki.

Hapa zoezi la makabidhiano ya zawadi ikiendelea.


0 Response to "WANANCHI WA KATA YA KERENGE-KOROGWE WAPATA MASHINDANO YA MALARIA CUP"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.