Habari za hivi Punde

MALARIA -CUP YALINDIMA WILAYANI KILINDI MKOANI TANGA VIJANA WAONYESHA VIPAJI VYAO


Timu  ya mpira dogodogo FC iliyopo wilayani Kilindi mkoani Tanga ikiwa katika uwanja wa  Mabombwe kwa kuajiandaa katika ligi ya Malaria Cup iliyodhaminiwa na PSI-Tanzania kwa mkoa wa Tanga ambapo muandaaji wake ni kutoka ofisi ya Wakati  Sports Promoter  ikiwa mchezo huo ulianza kwa timu hiyo na Polisi Fc ya wilayani humo,timu ya Dogodogo ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuifunga timu ya Polisi  FC kwa njia ya penati   baada ya kutoka  magoli matatu kila timu  mpaka mwisho wa mchezo,utaratibu uliowekwa ni mtoano timu itakayofungwa itatoka katika mashindano lakini itapata zawadi ya mpira mmoja huku timu itakayokuwa bingwa itachukua  jezi seti moja na mpira hivyo wilaya ya Kilindi timu nane zimejitokeza kucheza ligi hiyo.

Hii ni timu ya  Polisi Fc iliyocheza na timu ya Dogodogo na kufungwa goli 4-3 kwa njia ya penati ,sasa imeondolewa na kusubiri zawadi ya mpira mmoja.

Ofisa michezo wa  halmashauri ya wilaya ya Kilindi  Beno Haule akikagua timu ya Dogodogo  katika uwanja wa  Mabombwe tayari mwa mchuano.


Ofisa michezo Beno Haule  wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi akifungua  mashindano ya ligi ya Malaria Cup yaliyodhaminiwa na PSI  mkoani Tanga,ambapo alimshukuru Promoter Sophia Wakati kuwakumbuka katika sekta ya michezo kwa vijana wao,hivyo alimtaka kuendelea kuleta mashindano zaidi kwani wilaya hiyo ina timu zaidi ya 100 kinachosumbua ni kukosa wadhamini wa kuendeleza michezo,pia amesisitiza dhana nzima ya kufuata kanuni,taratibu na sheria katika ligi hiyo,

Sophia Wakati akimkabidhi ofisa michezo wa halmashauri ya wilaya ya Handeni jezi na mipira kwa timu nane zitakazoshiriki .

Makabidhiano ya zawadi za jezi na mipira yalifanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo na kuwakutanisha viongozi wa timu shiriki kushuhudia

Mjumbe wa kamati tendaji aliyevaa suti nyeusi   Mbaruku  Mangole akijitambulisha kwa viongozi wa vilabu ambao hawapo pichani .

ukaguzi wa timu ukiendelea  baada ya ofisa wa michezo Beno Haule kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo.

Timu ya Polisi Fc  ikiwa pamoja na  viongozi wa wilaya.


Sophia wakati  kutoka ofisi ya  Wakati Sports Promoter akiongea na timu zote ambapo timu inayoonekana ni Polisi Fc huku akiwasihi  kuwa na nidhamu ndani ya uwanja kwa kufuata kanuni,sheria na taratibu za mpira,ambapo alieleza lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji kwa vjiana katika michezo,pia  mashindano hayo yamedhaminiwa na PSI -Tanzania mkoani Tanga kupinga ugonjwa hatari wa malaria "MALARIA HAIKUBALIKI", pia aliserma kuwa mashindano hayo sio mwisho yatakuwa endelevu kutoka kwa wadhamini mbalimbali naye yuko bega kwa bega kuhakikisha vijana wanakuza vipaji vyao kwa kupitia mpira wa soka.

Mbaruku Mangole ambaye ni mjumbe wa kamati tendaji chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kilindi (KDFA) akiwa mmoja wa mashuhuda wa zawadi zinazokabidhiwa kutoka ofisi ya Wakati Sports Promoter.

Viongozi wa vilabu vya mpira wa miguu wilayani Kilindi wakisikiliza  maelezo  yanayotolewa na  katibu wa chama cha mpira  wilayani Kilindi  Omary  Javu ambaye hayupo pichani.

Katibu wa chama cha mpira wa miguu wilayani kilindi  (KDFA)   Javu Omary  akiongea na  viongozi wa vilabu ,huku akishukuru ofisi ya  Wakati Sports Promoter  kwa kuleta mashindano ya Malaria Cup wilayani humo.

Ofisa wa michezo halmashauri ya wilaya ya Kilindi  Beno Haule akifurahia zawadi za jezi na mipira huku akiwaonyesha viongozi wa vilabu waliohudhuria  katika ukumbi wa halmashauri hiyo baada ya Sophia Wakati kukabidhi.

Ukaguzi wa timu ukiendelea  tayari kwa kuingia uwanjani.

Timu zimeonyesha  shauku ya kucheza kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu huku wakifurahia mashindano ya ligi ya Malaria Cup.

Viongozi wakiangalia mechi inavyokwenda katika uwanja wa Mabombwe wilayani Kilindi mkoani Tanga ambapo ofisi ya Wakati Sports Promoter imekuwa ikikuza michezo na kuibua vipaji ndani ya mkoa wa Tanga,ambapo mashindano yaliyopo sasa ya Malaria Cup yamedhaminiwa na PSI mkoani Tanga Lengo kuu ni kutoa elimu juu ya kupinga ugonjwa wa Malaria.

Sophia Wakati   akiwa meza kuu kabla ya  kuwakabidi viongozi wa michezo wa  halmashauri ya wilaya ya Kilindi zawadi za jezi na mipira.

Mashabiki wakiwa nje ya uwanja wakiangalia timu zinavyocheza uwanjani.

Uongozi kutoka ofisi ya Wakati Sports Promoter   na viongozi wa michezo wilaya ya Kilindi.
Viongozi wakipongezana kwa kupokea jezi  na mipira.

Viongozi wa   michezo wilaya ya Kilindi  wakiangalia zawadi  kwaajili .
KARENY. Powered by Blogger.