TAARIFA tulizozipata mchana huu kutoka mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro, zinasema jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha
katika mahakama ya kijeshi askari wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa
kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu wa
shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.
Habari zinasema kuwa,askari huyo ambaye septemba 21 mwaka huu
alimfungia kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na
baadaye wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki, aliumia kwenye moja
ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi.
Kaimu kamanda wa liposi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita, pamoja na
kukiri kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa
kuweka wazi kama askari huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.
Kamanda Koka amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, jeshi la
polisi linafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama
itabainika,askari huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua
zaidi kuchukuliwa.
Pamoja na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari
huyo,taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi hiyo zinadai
kuwa,kuna juhudi za makusudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka
kukwamisha mashitaka ya kijeshi dhidi ya askari huyo.
Taarifa zinadai kuwa,polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini
moshi,wanajenga ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka
kulimaliza suala hilo kienyeji huku hali ya mwanafunzi huyo ikielezwa
kuwa mbaya kutokana na miguu yake kuvimba.
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu wa
0 Response to "POLISI ALIYEMFUNGIA MWANAFUNZI GUESTI ASHITAKIWA KIJESHI -KILIMANJARO."
Post a Comment