Mwili
wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke
na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa
gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha
ndani ya nyumba yao .
Katika
dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano
iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia
hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na
kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.
Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa
kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua
kuangalia kujua kinachoendelea.
Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na kuwataarifu wenzake.
Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki,
na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu
inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu
bila onyo, maumivu, wala kujijua.
Utadhani unapata usingizi na kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta.
Uthithubutu kupika kwa kutumia mkaa ndani ya nyumba bila kufungua
madirisha, au kuwasha jenereta ndani ya nyumba, au kuwasha gari katika
“garage” wakati madirisha na milango imefungwa; maana hiyo ni sawa na
kucheza na kifo.
Gesi ya carbon monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa
na wanyama, ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiy
0 Response to "JENIRETA LALIPUKA LAUA FAMILIA CHANZO BABA MWENYE NYUMBA KUFICHA NDANI KUOGOPA WIZI"
Post a Comment