WANAFUNZI wawili
wa shule za msingi za Nyabisara (Murito) na Kerende Kata ya Kemambo
wilayani Tarime, Mara wameumwa hadi kuondolewa nyama zao za miguu na
mamba walipokwenda kuoga maji ya mto kwa nyakati tofauti.
Wanafunzi
hao ni Penina Joseph Mangure (11) wa darasa la nne Shule ya Msingi
Nyabisara katika Kijiji cha Murito ambaye ni mtoto wa mwenyekiti wa
kijiji hicho, Joseph Mangure na Stephano Stephano (11) pia wa darasa la
nne Shule ya Msingi Kerende.
Taarifa
za wanafunzi hao kukutwa na mkasa huo zilifikishwa katika Kituo cha
Polisi Nyangoto (Nyamongo) na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
Akizungumza
hivi karibuni, baba wa Penina alisema mwanaye aliokolewa na wananchi
baada ya kupiga kelele wakati akiwa ameshikilia nyasi zilizomsaidia
kushindwa kutumbukizwa majini na mamba huyo ambaye alikwenda na kipande
cha nyama ya mguu wa kushoto.
Kwa
upande wake mtoto Stephano alidaiwa kukutwa na tukio hilo alipokuwa
akioga maji ya mto huo wakati akichunga ng’ombe wa nyumbani kwao.
Mtoto
huyo alifanikiwa kuokolewa na wasamaria wema alipokamatwa na mamba huyo
baada ya kupiga kelele na kufanikiwa kumtoa mguu katika mdomo wa mamba
lakini akiwa ameshamnyofoa kipande cha nyama mguu wa kushoto pia.
Mwenyekiti
huyo alisema tangu Januari hadi Oktoba mwaka huu, watu watano wa kijiji
chake wameshapoteza maisha baada ya kuliwa na mamba kwa nyakati tofauti
huku wengine takribani 100 wakijeruhiwa.
Pia
mwenyekiti huyo alisema mto huo kupita katika makazi ya watu ni tatizo
na kwamba kila mara wananchi wanapopatwa na adha hizo huwasilisha
taarifa katika Halmashauri ya Wilayani Tarime kupitia kitengo cha
wanyama pori kwa ajili ya kusubiri hatua zaidi.
Alimuomba
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu kuhakikisha inawafidia
wote waliojeruhiwa au kupotezewa maisha na mamba hao.
Watoto
hao bado wanasota majumbani mwao baada ya tiba ya awali huku wazazi wao
wakitafuta fedha ili wapelekwe Hospitali ya Bugando, Mwanza
0 Response to "WANAFUNZI WAWILI WATAFUNWA NA MAMBA HUKO TARIME"
Post a Comment