KADA WA CCM WILAYANI MASWA MKOANI SIMIYU STANSLAUS NYONGO.
WANANCHI na wadau mbalimbali katika
wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu wametakiwa kujitolea katika masuala ya elimu na
maendeleo na kuacha kuchangia mambo mengine yasiyokuwa na tija.
Hayo yalielezwa jana na Kada wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Maswa ,Stanslaus Nyongo katika mahafali ya
kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Shishiyu iliyoko wilayani humo.
Alisema wazazi wanatakiwa
kuhakikisha wanawarithisha watoto wao elimu na si kitu kingine kwani kufanya
hivyo kunawaandalia maisha yaliyo bora.
“Mafanikio ya wanafunzi wetu ni
mafanikio kwa taifa hivyo tunatakiwa kuhakikisha wanapata elimu iliyo bora kwa
kushirikiana kwa pamoja,” alisema
Nyongo ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali hayo alisema kuwa wazazi hao wana wajibu na ulazima wa
kuhakikisha kwamba watoto waowanawasimamia vyema katika kupata elimu bora
itakayotoa mwanga wa kimaisha katika hatma yao ya baadaye.
Alisema jukumu la kuhakikisha mtoto
anapata elimu si la serikali pekee bali ni wazazi na wadau mbalimbali kuungana
kwa pamoja.
“Urithi pekee ambao mzazi au taifa
linatakiwa kuutoa kwa watoto ni elimu nanyi watoto mnatakiwa kuacha anasa na
kuweka akili zenu katika masomo,acheni kucheza michezo isiyokuwa na tija kama
‘game’ na matumizi ya simu ambayo yanawaathiri kwa sehemu kubwa ili mtakapofika
wakati wa kufanya mitihani mfanye vizuri”.Alisema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa shule hiyo, Godlisten Kabarata alisema
kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2006 ya Kata ufaulu umekuwa
ukiongezeka kwa wanafunzi wa kidato cha nne na kwa mwaka uliopita shule hiyo
ilishika nafasi ya kwanza ya katika wilaya hiyo kati ya shule 38.
Katika Mahafali hayo jumla ya
Shilingi 1,700,000/=zilikusanywa kwa ajili ya kuweka umeme katika vyumba vya
madarasa na nyumba za walimu ambapo mgeni Rasmi alichangia fedha taslimu
kiasi cha shilingi 500,000/= na wanafunzi 83 wakiwemo wavulana 53 na wasichana
30 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu.
|
0 Response to "WANANCHI WATAKIWA KUWAPA MAENDELEO YA ELIMU WATOTO WAO"
Post a Comment