Habari za hivi Punde

BAADHI YA ASKARI MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA SEMINA FUPI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)

Baadhi ya Askari  mkoani Shinyanga wakisikiliza moja ya semina iliyoandaliwa na mwamvuli wa mifuko ya jamii nchini SSRA ambapo semina hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa Ibanza hotel  huku wakiwa na  shauku kubwa ya kujua  changamoto zinazowakabili baada ya kujiunga na mifuko ya hifadhi mbalimbali.

Insp  Robert Mageta  wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga  akiuliza swali juu ya mafao wanayokatwa  katika mifuko mbalimbali  huku akieleza  baadhi ya miaka wanayokatwa  mafao hayaonekani.

WP  Rose   akitoa  ushauri kwenye mamlaka ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa  ni bora kungekuwepo na mfuko mmoja wenye kueleweka na kutoa mafao sawa kuliko ilivyo mingi na kuonekana kuna ubabaishaji ndani yake.

Baadhi ya askari wakiwa katika picha ya pamoja na  wakufunzi mara baada ya kumaliza semina  hiyo.

0 Response to "BAADHI YA ASKARI MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA SEMINA FUPI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.