Habari za hivi Punde

MAANDAMANO YALIYOFANYWA NA WANAWAKE WA UWT MANISPAA YA SHINYANGA LENGO KUPINGA UKATILI WA WATOTO.


BAADHI ya wakazi wa manispaa ya Shinyanga wakifanya maandamano ya kupinga  ukatili dhidi ya watoto ambayo yamekuwa yakifanywa na  baadhi ya waendesha daladala za baiskeli  kwa kuwafanyia watoto vitendo vya ubakaji huku wakiaachia ulemavu kwa kuwatoboa macho.


Wakazi hao waliokusanyana katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini  waliamua kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kutaka waendesha dalala hao wawe na usajili  maalumu wa kuwatambua au kuondoka kabisa na kuwepo kwa usafiri wa daladala za magari kama wafanyavyo  mikoa mingine.


Zoezi la maandamano  lilianza huku wakiimba nyimbo za kupinga ukatili wa watoto ambapo maandamano hayo yalipokelewa   na mkuu wa wilaya Annarose Nyamubi yalipofika ofisini kwake sanjari na mbunge viti maalumu Azzah  Hillali akiomba serikali kuangalia suala hilo ili kuweza kunusuru watoto ambao ni taifa la kesho.


0 Response to "MAANDAMANO YALIYOFANYWA NA WANAWAKE WA UWT MANISPAA YA SHINYANGA LENGO KUPINGA UKATILI WA WATOTO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.