BAADHI ya wajiriwa
katika sekta mbalimbali mkoani Shinyanga
wameitaka mamlaka ya mfuko wa
hifadhi ya jamii nchini (SSRA) kuzisimamia hifadhi zilizopo ili kuacha
kufanya kazi kwa kutapeli bila
kueleza viwango vya fedha wanavyokusanya hali ambayo imejidhihirishia
hata kipindi cha kustaafu kupokea mafao yao kidogo tofauti na wanavyotarajia.
Hata hivyo imebainika kuwa watumishi wapya wa serikali
hususani waajiriwa wapya kutoa fomu ambazo zimeshajazwa bila kutoa ushauri mzuri, hali ambayo inasababisha baada ya muda
wateja wao kujutia kujiunga na baadhi ya mifuko hiyo.
Changamoto hiyo
ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Annarose Nyamubi kwenye semina ya elimu juu ya hifadhi ya jamii kwa viongozi wa
mkoa wa Shinyanga na halmashauri ,ambapo
alisema baadhi ya mifuko haifanyi kazi zake kwa uwazi hivyo kuwatapeli watumishi hasa waajiriwa
wapya.
“Mifuko hiyo inatakiwa kufanya kazi zake kwa uwazi na kutoa
huduma iliyobora kwa wateja wao ili kuwahamasha watumishi wengine kutoka
serikalini,mashirika,taasisi na watu binafsi kujiunga ili kujiwekea akiba ya
uzeeni pamoja na mafao mengine ukiwemo uzazi na matibabu”alisema Nyamubi .
Alisema kuwa kitendo cha mtumishi kufanya kazi kwa muda wa miaka 30 na kufanananishwa na yule aliyefanya miaka mitano kinaumiza ikiwa leo hii gharama za maisha zinapanda kila kukicha
kinachotakiwa wasimamizi wa mifuko hii kwenda na mabadiliko ya hali halisi iliyopo.
Nyamubi alisema mfuko wa hifadhi ya jamii(NSSF) umekuwa
ukilalamikiwa na watumishi wengi kwa kushindwa kuboresha huduma zake, hali hiyo
inaweza kusababisha kukosa wananchama na malengo yao kutofikiwa na kutolea
mfano wakati wa mei mosi mabango mengi yalikuwa yakiulenga mfuko huo kwa
kuumiza watumishi katika mafao.
Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo kutoka (SSRA) Dar
es salaam ambaye ni afisa mipango na rasilimali watu Mohamed Nyasama,alisema mpaka sasa ni asilimia 4.5 ya watanzania wote ndiyo
wamejiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,idadi ambayo bado iko chini tofauti na
ambao hawapo kwenye mfumo wa ajira rasmi.
Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kutetea na kulinda
maslahi ya wanachama,wafanyakazi na wastaafu ili kuleta faida kwa wateja kwa
kuboresha uhakika wa maisha yao ya baadaye,kinga dhidi ya majanga kwa
watanzania na kukuza uwekezaji nchini.
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi alisema
utendaji mbovu wa baadhi ya mifuko unakatisha tamaa watumishi kujiunga na mifuko yao, kutokana na
kuona hali halisi jinsi wazee wastaafu wanavyohangaika kufuatilia mafao yao
wakati takwimu zote zipo lakini kwenye malipo inakuwa tatizo.
Naye Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya
wafanyakazi mkoa wa Shinyanga (TUCTA)Fue Mlindoko,alisema kero kubwa
wanazokumbana nazo ni mafao kutokuwa sawa miongoni mwa watumishi wakati
wakitambua tarehe za kuajiriwa na kustaafu kwao , lakini cha kusikitisha
inaoneka ofisi za hifadhi hizo haziweki
kumbukumbu nzuri ndio maana huwaomba tena uthibutisho wa kazi jambo ambalo limekuwa ni usumbufu.
.
0 Response to "MAMLAKA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YATAKIWA KUSIMAMI ILI KUONDOA UTAPELI UNAOFANYWA."
Post a Comment