Katika mikoa sita na wilaya 23 ,ambapo ekari 50 ,000 hazikuota zilizopandwa kwa kutumia mbegu ya quiton UK 91 na UK 08 ,ambazo zilifanyiwa utafiti katika chuo cha Ukiriguru jijini Mwanza na kuonekana zinafaa kwa kuwa na ubora mkubwa utakaosaidia kuongeza uzalishaji
Ufafanuzi wa tatizo la mbegu hizo kutoota kwa wakulima lilitolewa wakati wa ziara ya Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika wilayani Kishapu ambapo mkurugenzi wa huduma za usimamizi bodi ya pamba Tanzania James Shimbe,alisema katika mikoa inayolima pamba ni Mara pekee ndiyo ambayo haikuathirika kutokana na mbegu bora ambazo wanazalisha wao .
“Tulifuatiliaili kuona baadhi ya maeneo mbegu hizo kwanini zishindwe kuota, lakini kulibainika mambo mbalimbali ikiwa baadhi ya mifuko ya mbegu ilikutwa na fangazi na kuwa na unyevunyevu na kubadilika kuwa nyeusi,wakulima hawakupata elimu ya kutosha jinsi ya kupanda na utunzaji pia mbegu hizo ”alisema Shimbe.
Hivyo bodi ya pamba itahakikisha inatafuta njia sahihi ya kumaliza tatizo hilo ili lisiweze kujirudia kwa mara nyingine, kutokana na kusababisha hasara kwa wakulima na baada ya kubaini hali hiyo tani 3117 za mbengu zilisambazwa kwa wakulima ikiwa ni hatua ya kuwasaidia waweze kupanda tena.
Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi aliwatahadharisha viongozi wa serikali kuwa makini na wanasiasa kutokana na baadhi yao kugeuza zao hilo kuwa sehemu ya siasa wakati wanaopiga kelele wakichunguzwa hawana hata shamba bali wababaishaji.
Alisema mbegu za quiton zimefanyiwa utafiti na chuo cha Ukiriguru na kubaini kuwa zinaubora huku akisema tatizo liko katika usambazaji wa mbegu hizo, jinsi ya kutunza na upandaji kwani kampuni ya Quiton mkataba wake na wizara ni kuzalisha na siyo kusambaza.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Justine Sheka,alisema tatizo la mbegu kutoota ni kubwa kwani katika wilaya hiyo wakulima zaidi ya 13OO mashamba yao hayakuota na hivyo kupata hasara ya zaidi ya billion 1.6.
0 Response to "ZAIDI YA WAKULIMA 14,000 WAMEBAINIKA KUPATA HASARA KWA KUTUMIA MBEGU ZISIZO NA MANYOYA NA KUTOOTA. VIZURI"
Post a Comment