MRADI wa mbwawa la umwagiliaji katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule halmashauri ya wilaya Shinyanga umeingia sura mpya mara baada ya naibu waziri wa kilimo,chakula na ushirika Godfrey Zambi kuutembelea na kujionea hali halisi ya kutokamilika kwake ingawa mkandarasi ameongezewa muda huku akisikitishwa na uongozi ngazi ya kanda,mkoa na wilaya kutoshirikishwa na kuutambua.
“Nina kiri baadhi ya miradi imetumia fedha nyingi zaidi ya shilingi million 200 lakini miradi hiyo imefanywa vibaya ,pia serikali ilidhamiria kuweka mradi huu hapa hali imeonekana mkandarasi ndio hovyo na kutokuwa na uwazi kwenye mradi, ikiwa uongozi wa ngazi mbalimbali unaotegemewa haujashirikishwa.”alisema Zambi.
Ambapo waziri huyo mara baada ya kujionea alipewa maelezo na injia wa skimu ya umwagiliaji Godrey Mbwambo kuwa mkataba wa mradi huo ulifungwa tarehe 15/02/2013 kati ya katibu mkuu na wizara ya kilimo chakula na ushirika na mkandarasi aitwaye SYSCON BUILDERS wa jijini Dar-es-salaam chini ya mhandisi mshauri CODA AND PARTERS ya Kenya baada ya kufunga mkataba mkandarasi alitakiwa kuanza kazi mwezi mmoja baada ya kufunga mkataba huo.
Mbwambo alisema kuwa mradi huo ulilenga kuwanufaisha wakulima na wafugaji kutoka vijiji viwili vya Ishololo na Tindeng’hulu ambao ungeweza kunufaisha wakulima zaidi ya 1500 na kiasi cha hekta zipatazo 500 zingeweza kumgwagiliwa na maji kutoka katika bwawa hilo.
“Mradi huu ambao unafadhiliwa na mradi wa uwekezaji katika sekta ya kilimo wilaya (DASIP) imechangia kiasi cha zaidi ya shilingi millioni 740 na mfuko wa umwagiliaji (DIDF) kwenye mradi huo imechangia kiasi cha shilingi millioni 200 na kufanya jumla ya gharama ya mradi ya shilingi millioni 940”alisema Mbwambo.
Pamoja na maelezo hayo naibu waziri huyo alitaka kupata majibu kutoka ofisi ya kanda ambao walidaiwa kuwa wahusika wa mradi huu,pia alisema kushindwa kutekelezeka fedha hiyo ninavyofahamu itarudi benki ya Afrika (AFDB) kwa kuwa mradi wa DASIP uliisha muda wake 31/12/2013, ingawa inaelezwa aliongezewa muda na kushindwa kukamilisha pia.
Zambi alisema kuwa kweli katibu wa wizara ndio aliyesaini mikataba yote hivyo yatahitajika mazungumzo ofisini,,ikiwa mhandisi wa umwagiliaji kutoka ofisi ya kanda ya ziwa iliyopo jijini Mwanza Ebeneza Kombe alisema kuwa mradi huo uliandikiwa jumla ya shilingi billion 1.2 katika bajeti yake ya mwaka 2013 lakini hazikuja katika ofisi hizo ililazimu tena kuandika maandiko mengine kwa kuanza upya.
Hata hivyo mbunge viti maalum Azzah Hilali alimueleza naibu waziri kuwa ofisi ya kanda wanyooshe maelezo mradi huo wao kama halmashauri na mkoa walielezwa hawahusiki bali ni ofisi ya kanda na wizara ikiwa wakulima wamekuwa wakilalamika kushindwa kutekelezeka kwa wakati huku mkandarasi hana vifaa matokeao yake kufanya shughuli zake binafsi vijijini hapo.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Kiyungi alisema kuwa kiasi cha shilingi millioni 200 zilizotoka DIDF na kuhamishiwa akaunti ya mradi wa DASIP Mwanza wao kama halmashauri walikuwa wanaomba fedha hizo zirudishwe kwenye akaunti ya halmashauri ili ziweze kuendeleza shughuli za miradi ya umwagiliaji.
Diwani wa kata hiyo Amina Bundala alisema kuwa alitakiwa kuanza kazi tarehe 15/03/2013 na kazi hii ilitakiwa ifanyike ndani ya siku 240 sawa na miezi nane ,licha ya kuongezewa muda sisi viongozi tumeonekana waongo sababu tangu mwezi huo mifugo inakunywa matope badala ya maji wakulima wamevurugiwa mashamba yao ikiwa bwawa hilo linahitaji kuhudumia kata za Bukene,Imesela Usule na Tindenhulu.
Mradi huu uliibuliwa na wananchi wenyewe katika bajeti ya kijiji ya mwaka 2011/12 kwa kutaka bwawa kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mpunga ikiwa walikuwa wakikosa maji ya kutosha kwa kuliendeleza zao hilo na kupata mavuno ya kutosha huku halmashauri ikipata pato la ndani zaidi kupitia ushuru za zao la mpunga.
0 Response to "MRADI WA BWAWA LA ISHOLOLO WAMSIKITISHA NAIBU WAZIRI WA CHAKULA KILIMO NA USHIRIKA ALIPOPATIWA MAELEZO JUU YA KUKWAMA KWAKE"
Post a Comment