WAJASILIAMALI
manispaa ya Shinyanga wamepatiwa
elimu juu ya kujiunga na mfuko wa
hifadhi ya jamii ili kuweza kuboresha maisha yao na kuondoa dhana ya mifuko hiyo kuwa inawahusu waliopo kwenye sekta rasmi
pekee kama ilivyo kuwa awali.
Kwa sasa mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya
mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) imeamua kutoa fursa hata kwa
wajasiliamali wanaofanya biashara
ndogondogo kujiunga na mifuko hiyo kwa
mujibu wa Hifadhi ya mifuko ya jamii ni haki ya kila mtu kujiunga nayo, haki
hii imeanishwa katika ibara ya 11 (1) ya
katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na sera ya taifa ya hifadhi ya jamii
ya mwaka 2003.
Akitoa elimu kwa wajasiliamali hao mwanasheria mwandamizi
wa mamlaka hiyo Salma Maghimbi kutoka makao makuu Jijini Dar es slaam alisema
moja ya wajibu wa mamlaka hiyo ni kutoa elimu kwa watanzania wote walioajiriwa
na kujiajiri wenyewe ilikupanua wigo kwa wananchi kujiunga na mifuko ya hifadhi
ya jamii.
Maghimbi alisema mamlaka hiyo imeruhusu uandikishaji wa
wanachama kutoka sekta isiyo rasimi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya
jamii mbalimbali hapa nchini ambao ni wakulima,na wafanyabishara ndogondogo
(Wajasiliamali) kwa lengo la kupanua wigo mpana wa hifadhi ya jamii
ulioendelevu na wenye huduma bora kwa kila mtanzania.
“ Changamoto ya
sekta ya hifadhi ya jamii iliopo inaonyesha takwimu kuwa wananchi waliokatika sekta rasmi wanaokadiliwa kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta ya hifadhi ya
jamii na watanzania waliowengi ambao wapo katika sekta isiyo Rasmi wamekuwa
hawanufaiki na mifuko hiyo na kuwafanya kuwa na maisha magumu hasa pale
wanapostaafu”.
Maghimbi alitaja faida zinazo patikana katika mifuko hiyo ya
hifadhi ya jamii kuwa ni mafao ya uzeeni, ulemavu, kuumia kazini, pamoja na
kupata mikopo ya kuendeshea biashara na kukuza mitaji yao hali ambayo itakuza
uchumi wanchi na kuongeza pato la taifa.
Akizungumza katika utoaji wa elimu kwa wajasiliamali hao ofisa
Biashara wa manispaa ya shinyanga Erasto Mabina alitumia fursa hiyo kuwataka
wafanyabiashara wa manispaa hiyo kujenga tabia ya kukata leseni za biashara ili
kufanya biashara zao kiuhalali na kuchangia pato la serikali, fedha ambazo
zitasaidia kuendesha miradi ya maendeleo.
kwa upande wa wajasiliamali hao kwa nyakatitofauti
waliiomba mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii hapa nchini kuboresha huduma zao kwa
wananchama na kuacha ubabaishaji na usumbufu ambao umekuwa ukilalamikiwa na
baadhi ya wanachama waliojiunga na mifuko hiyo.
Baadhi ya wajasiliamali wenzao Restuta Joseph na Ester
Paulo waliishukuru Mamlaka hiyo ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya mifuko ya
hifadhi ya jamii (SSRA ) kuwapa elimu na uelewa juu ya umuhimu wa
kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo watatumia vyema elimu hiyo kujiunga.
0 Response to "WAJASILIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA WAPATIWA ELIMU YA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI."
Post a Comment