Habari za hivi Punde

WADAU WA AFYA MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA TAARIFA KUHUSIANA NA UZAZI WA MPANGO KATIKA JAMII AMBAPO MKOA WA SHINYANGA UMEFIKIA ASILIMIA 12.5 KWA WANAOTUMIA NJIA YA UZAZI WA MPANGO.


Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli  Kapologwe akielezea wadau wa masuala ya afya mkoani humo jinsi ya mikakati ya uhamasishaji  wa uzazi wa mpango katika jamii ambapo kimkoa umekuwa  na asilimia 12.5 ya idadi ya watu wanao tumia uzazi wa mpango kwa njia ya kisasa.



Wadau wa afya mkoani Shinyanga  wakisikiliza taarifa iliyotolewa  dhidi ya  wizara ya afya huku wakilalamika  kuhusiana na takwimu zinazotolewa ,ambapo wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii  jinsi ya utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango ikiwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakilalamika na kudai kuwa  njia hizo zimekuwa zikiwaletea madhara  ikiwa wataalamu hao wamesema sio kweli ni njia bora  na kila mmoja ana uhuru wa kuchagua anayoipenda.


Wadau wa afya mkoani Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa mkuu wa mkoa ambapo wakijadiliana  suala la uzazi wa mpango huku aliyesimama ni Dkt Gregory  Kamugisha kutoka chuo kikuu cha John Hopkins kilichopo nchini Marekani kwa tawi la Dar-es-salaam huku akieleza kuwa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango kwa mkoa wa Shinyanga upo chini ambapo imeelezwa kuwa  wanawake waishio vijijini kwa wastani  ni asilimia 6.1 huku mijini ni asilimia 3.7 ya wanawake wenye watoto kwa tawkimu zilizotolewa na wizara ya afya mwaka 2010.


0 Response to "WADAU WA AFYA MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA TAARIFA KUHUSIANA NA UZAZI WA MPANGO KATIKA JAMII AMBAPO MKOA WA SHINYANGA UMEFIKIA ASILIMIA 12.5 KWA WANAOTUMIA NJIA YA UZAZI WA MPANGO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.