Habari za hivi Punde

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAMEFANYA UCHAGUZI NAIBU MSTAHIKI MEYA DAVID NKULILA AMERUDIA NAFASI YAKE KWA KUPIGIWA KURA NA KUPATA 15 HUKU MGOMBEA WA CHADEMA KWA NAFASI HIYO GEORG KITALAMA AKIPATA KURA 6.



Kikao cha kwanza cha baraza la madiwani manispaa ya Shinyanga ambacho kimekaa kwa  kumchagua  naibu meya wa manispaa hiyo kwa mujibu wa kanuni na sheria za   TAMISEMI ikiwa vyamba  viwili ndani ya manispaa hiyo ambavyo ni Chadema na CCM walisimamisha wagombe wao kwa mujibu wa sheria na taratibu ambapo chama cha mapinduzi kilimrudisha  David Nkulila kuwa mgombea tena katika kiti hicho alicokuwa akikiongoza kwa miaka mitatu mfululizo huku mgombea  kutoka chadema  George Kitalama akisimamishwa kugombea nafasi ya unaibu meya ambapo zilizpigwa kura,katika baraza hilo katika picha hapo juu ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselmo Tarimo na katibu tawala wilaya Boniface Nchambi wakihudhuria baraza hilo na kufuatilia kwa umakini namna taratibu zinavyo kwenda.


Wajumbe,wataalamu na wageni waalikwa wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya  unaibu meya wa manispaa David Nkulila alipokuwa akijinadi kwa wajumbe ili wampigie  kura.


Diwani wa kata ya kitangili  kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) George Kitalama  ambaye aliteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya naibu meya wa manispaa ya Shinyanga  ambapo hapo pichani anavyoonekana alikuwa akijinadi wa wajumbe wampigie kura.


Diwani wa kata ya Ndembezi ambaye alikuwa ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila  kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi akiwa amesimama mbele ya wajumbe kwa kuomba kura ili waweze kumchagua,lakini aliweza kuchaguliwa baada ya zoezi la kujinadi kukamilika na kupata kura kumi na tano ambapo alimshinda  mpinzani wake Kitalama kwa kupata kura sita kati ya wajumbe 21 waliopiga kura pia hakuna kura yoyote liyohalibika.


Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa  msimamizi wa uchaguzi ambaye hayupo pichani.


Msimamizi wa uchaguzi huo  Daniel Mkumbo ambaye alikuwa akitoa maelekezo namna ya upigaji kura utakavyokuwa.


Diwani wa chadema kata ya Ndala George Sungura akiwa amesimama  kwa lengo la kumuuliza maswali mgombea unaibu meya wa manispaa David Nkulila kuwa   ikiwa amekuwa na ubaguzi pindi akichaguliwa ataweza kuleta mshikamano kwa wataalamu na madiwani ambalo limekuwa ni tatizo katika utendaji kazi kwa kipindi  alichokuwa   naibu meya.


Utaratibu wa upigaji kura kwa mtindo huo madiwani wa chadema waliukataa huku wakidai kuwa kura zinaweza kuchakachuliwa  ikiwa walianza kupiga na baadaye kurudiwa tena kwa utaratibu walioutolea maoni wa kunyanyuka na kukubaliana kwa wote.


Gaudioz Mwombeki ambaye ni mwandishi wa vikao katika manispaa akiwa amebeba sanduku la kupigia kura ambapo wajumbe kutoka  chadema walikataa upigaji kura  kwa  utaratibu huo huku wakitoa maoni kuwa kura hizo ni za siri hivyo ni bora kila mmoja akanyanyuka na kupiga kura mwenyewe bila kumpasia  mtu mwingine  karatazi ya kupigia kura .


Mbunge viti maalumu kutoka chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Rachal Mashishanga  akisikiliza kwa umakini utaratibu wa upigaji kura ndani ya ukumbi huo.


Sanduku la kupigia kura ambalo limeandaliwa katika ukumbi  uliokuwa ukifanyika kwa baraza  kuu la mwaka.


0 Response to "BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAMEFANYA UCHAGUZI NAIBU MSTAHIKI MEYA DAVID NKULILA AMERUDIA NAFASI YAKE KWA KUPIGIWA KURA NA KUPATA 15 HUKU MGOMBEA WA CHADEMA KWA NAFASI HIYO GEORG KITALAMA AKIPATA KURA 6."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.