Habari za hivi Punde

MBUNGE WA JIMBO LA SOLWA ATATUA BAADHI YA KERO,IKIWEMO HUDUMA YA USAFIRI KWA WAGONJWA.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum akiwa katika  mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji na kata ya Nyida   ambapo alizungumza kuwamalizia kero zinazowasumbua ikiwemo ukosefu wa kituo cha afya katika kata hiyo ambapo inawafanya wakazi hao kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita kumi kutafuta matibabu kwenye kata za jirani jambo ambalo alionyesha kukerwa na kuahidi kukamilisha ujenzi uliobaki ambapo wananchi hao kwa nguvu zao walianza michango juu ya ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho ili kuweza kuondoa changamoto ya kutembea umbali huo.licha ya  zahanati au kituo cha afya kutokuwepo kumekuwepo na changamoto ya uhaba wa maji nayo ameahidi kukabiliana nayo kutokana na fedha zilizotengwa ndani ya halmashauri kupitia mradi wa fedha kutoka benki ya dunia.

Hapa mbunge huyu akiongelea suala la kilimo cha umwagiliaji baada ya kuulizwa maswali kuhusu  mpango wa mto manonga umefikia wapi ikiwa wanautumia kwa mikoa ya Tabora na Shinyanga  hivyo wanaomba kupatiwa majibu  kuhusu mto huo mmiliki halali ni nani kwani hapo baadaye utaanza kuleta mgogoro,pia changamoto ya umeme wananchi walihitaji umeme ikiwa wanatumia sola inayotumia gharama kubwa  hivyo walimuomba kuwaletea umeme ndani ya kata hiyo.

Hapa wakiwa katika kijiji cha Masekelo kata ya Bukene   katika halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alijiandaa kuweka jiwe la msingi kwenye  ujenzi wa mbweni la wasichana ambalo halipo pichani linalodaiwa hapo lilipofikia usawa wa lenta kugharimu jumla ya shilingi millioni 36 zilizotolewa na halmashauri  huku bado kiasi cha shilingi millioni 12 ili kuweza kukamilisha ujenzi huo ambapo lilikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 40.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum akiendelea kuongea katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji  na kata ya Nyida.

Hapa akiendelea  kujibu maswali aliyoulizwa.

Gari hili amelitoa  mbunge huyo kwaajili ya  kuwabeba wagonjwa walio mahututi,wajawazito na wale watakao pata ajali  huku akisisitiza kuwa huduma hiyo itatolewa bure na mafuta yatakuwepo ya kutosha  atakayependa kutoa pesa ametaka mwenyewe,ikiwa baadhi ya wananchi walidai kuwa gari hilo lilikuwa likibeba wagongwa kwa kutozwa kiasi cha shilingi 40,000 hadi 60,000  ambapo walikuwa wakielezwa gaharama hizo ni kwaajili ya mafuta hali hiyo iliwafanya walio wengi kukosa kiasi hicho cha pesa na kufanya idadi kubwa ya wagonjwa kuzidiwa njiani na kupoteza maisha wakiwemo watoto na mama wajawazito.

Gari hii iliharibika hapo awali na kukaa muda mrefu bila matengenezo hivyo mbunge aliamua kutengenea gari hilo kwa kiasi cha shilingi miliioni 7.5  na kulifanya liwe zima tena pia aliwakabidhi wananchi wa kata ya Usule  huku akiwapa angalizo juu ya utumiaji wa gari hiyo na kuwaeleza kuwa ni bure usafiri.

Ngoma aina ya waswezi ikiburudisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Igalamya kata ya Usule

Mbunge Azzah Hilali alisimama na kuongelea kukerwa na baadhi ya wanaume kuwapatia mimba wasichana wa shule huku wazazi au walezi wa pande mbili kukutana na kumalizana kinyemela  hilo limekuwa ni tatizo hivyo kuna sheria inayoundwa mwanafunzi akipata mimba wazazi wote wa pande mbili wanashitakiwa mahakamani kwani  wanapofanya hivyo wanamnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu bora na kuendeleza wimbi la umasikini kwani hata wewe mzazi ukipewa ng'ombe tano hazina uthamani kama elimu atakayo ipata mtoto wa kike  katika maisha yake.

Mbunge Salum  akiendelea kuongea kwenye mktano wa hadhara.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mohamed Kiyungi akimpatia vielelezo mbunge wa jimbo hilo kutokana na changamoto zilizoulizwa  ili kuweza kuzipatia majibu katika mkutano huo.

0 Response to "MBUNGE WA JIMBO LA SOLWA ATATUA BAADHI YA KERO,IKIWEMO HUDUMA YA USAFIRI KWA WAGONJWA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.