Jeshi la Polisi kikosi
cha usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Nchi
kavu na Majini SUMATRA limeanzisha mkakati wa kuwafungia leseni madereva
watakaobanika kuendesha magari huku wakiwa wanazungumza na simu za
mkononi.
zoezi
hilo limekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwepo kwa ongezeko la ajali
za barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe ambao unasababishwa na
unywaji wa pombe,kuchoka na kuzungumza na simu hizo.
Takwimu zinaonyesha kuwa
kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali barabarani kwa mwaka 2013
sawa na asilimia 1.1 tofauti na mwaka 2012 ambapo matukio yalikuwa
23,578.
Kwa mwaka huu kati ya
januari hadi June idadi ya ajali zilizoripotiwa zilikiwa 8,405
zilizosababisha vifo 1743 na majeruhi 7,523 hali ambayo Kamanda Mpinga
anasema ipo mikakati mbadala ya kukabiliana na hali hiyo.
Inatajwa kuwa madereva
wengi hawana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara,inaelezwa kuwa
magonjwa ya macho,kisukari pamoja na shinikizo la damu pia linachangia
ajali nyingi.
Kampuni ya Bia Tanzania
TBL itatumia shilingi milioni 800 katika kufanikisha zoezi la kupima
afya za madereva katika vituo vitatu vya afya vya Msata Mkoani
Pwani,Mikese Mkoani Morogoro pamoja na Makuyuni Mkoani Arusha lengo
likiwa ni kuepukana na ajali
0 Response to "DREVA ATAKAYE ENDESHA GARI HUKU AKIONGEA NA SIMU KUKIONA;"
Post a Comment