Jaji
anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius,
amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu
la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp.
Hata
hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi
kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake
Reeva.
Pistorius
alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana
lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa
amevamia nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha
mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe
Reeva baada ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga
risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.
via>>BBC
0 Response to "MWANARIADHA AMBAYE ALIMUUA MPENZI WAKE ATETEWA,IKIWA YEYE WEMYEWE AMEKIRI."
Post a Comment