Nchini
Tanzania kuna makabila mengi ambapo baina yake,kuna utani wa jadi
miongoni mwao.Utani huu wa jadi upo karne na karne kabla hata nchi yetu
haijawa chini ya utawala wa kikoloni,na sijui ulitokea wapi?Na kabila
ambalo linaloongoza kuwa na watani wengi kutoka maeneo karibu yote
nchini,ni kabila la Wasukuma na wenzao Wanyamwezi.
Zama
hizo hadi kufikia mwanzoni wa uhuru wa Taifa letu utani wa jadi ulikuwa
na nguvu.Kila mmoja alimdhihaki na kumkejeli ama kumsema hata kumcheka
mtani wake mbele ya kadamnasi,kulikuwapo na vituko na majigambo
yaliyofanyika ama katika ngoma za jadi na kwenye vilabu vya pombe za
asili ambayo yalileta burudani ya aina yake.
Lakini utani huo wa jadi katika karne tulionayo,umekuwa hasi tofauti na zama za mababu na bibi zetu,sababu kubwa ikiwa ni mabadiriko ya sayansi na teknolojia.Utandawazi umekuwa athari kubwa kwa Jamii ya Watanzania kubeba asili yetu na kutawaliwa na tamaduni za kutoka nchi za Magharibi.
Zama
hizo za karne ya kumi na Tisa kurejea nyuma,Makabila ya Watanzania
yalithamini utamaduni huo wa kimila ambao uliwafanya watu kuambiana ama
kutendeana jambo lolote katika kipindi cha furaha na majonzi pasipo
chuki.Masihara yaliofanyika yalidumisha Mila na desturi ya kila kabila
la Muhusika.
Nyakati
zingine;Dhihaka hizo ziliambatana na faini,hidaya na hata mchango
kulingana na Nasaba moja hadi nyingine,kuwa na tukio la burudani ama
huzuni,au katika mfumo wa maisha ya kila siku,Mmoja kujisahau na kutenda
jambo litakalotoa faida ya hidaya kwa watani zake.
Mzee wa
kabila la Kingoni;Andrew Chitete {75}mkazi wa kitongoji cha Kasela Kata
ya Malunga wilayani Kahama,ameonekana kutoathirika na Utandawazi uliopo
kutokana na mfumo wake wa Maisha kuhakikisha anaendeleza mila na
desturi hizo za Mababu na Mabibi,kwa kinywa chake kutawaliwa na maneno
ya utani usioleta Ufidhuli kwa mtu wa Jinsi na umri wowote ilimradi
akijilidhisha ni mtani wake.Japo dhihaki zake kuna kipindi zilitaka
kumletea athari.
Amekuwa akijitokeza kufanya utani katika hadhara mbalimbali na
kuleta burudani ya aina yake na kipindi kingine kufanya tukio la
kuogofya ,ambapo matukio hayo mara nyingi amekuwa akiyafanya misibani
.Kama kutumbukia kaburini na kukumbatia sanduku la marehemu mtani wake lisifukiwe kukamilisha maziko hadi pale watani wake wanapompatia fedha ndipo huruhusu kukamilisha maziko hayo.Ufyosi wa namna hii haufanyiki maeneo mengi nchini na haujapata kutokea karibu robo karne sasa.
Mzee Chitete hufanya utani kwa watu ambao amejiridhisha kuwa ni watani zake wa jadi,huku lengo la ufyosi wake ni kudumisha Mila na asili ya Mtanzania.
Anasema;
“Ni vyema tukumbuke utani wetu wa jadi,ambao wazee wetu wa zamani
walikuwa wakiutenda pasipo kupotosha ambapo katika misiba ilisaidia
kupunguza machungu ya wafiwa.Na utani kama huu nimeufanya mara nyingi
hata kwenye maziko ya mama yake na Jaji Ihema yaliyofanyika Kata ya
Isagehe wilayani Kahama,nilitwaa Mishumaa yote na kuzuia maiti isizikwe
katika kaburi lililoandaliwa na kudai nataka kuusafirisha mwili wa
marehemu kuupeleka kwetu Songea kuuzika,nilipochangiwa fedha niliruhusu
maiti kuzikwa.”.
“
Utani unatambulika Kisheria ndio maana katika Maziko ya mzazi wa Jaji
Ihema ilipotaka kutokea vurugu kwa baadhi ya watu wasioelewa utani
kutaka kunishushia kipigo,Jaji aliwazuia kwa kuwaeleza kuwa nina
haki,huku akiwa miongoni mwa waliochanga pesa ili niruhusu maiti
izikwe,”Alisema Mzee Chitete.
Alikanusha
kuitumia misiba ya makabila ya Watani wake kama ni miongoni mwa mradi
wa kumuingizia kipato kwa kubainisha kuwa pesa anazochangiwa pindi
anapozuia maziko huzitumia kununua bidhaa mbalimbali kama
Mchele,Unga,Chumvi,Sukari,Dagaa,Maharagwe na vinginevyo ambavyo
huvipeleka kuwapa pole Wafiwa.
Mzee
Chitete alisema ni ada yake kufanya ufyosi kwa Mtani wake katika
mazingira yoyote yale,wakati wa raha,wa kawaida na vipindi vya misiba na
kukisisitizia kizazi kilichopo kuuenzi Utamaduni wa makabila yetu kwa
kutokuwa watumwa wa fikra kwa kuthamini Mila na Desturi za Ughaibuni na
Ulaya.
Tumo
katika kifungo cha fikra, ndio maana maadili kwa vijana wa leo ni
ruya,Utumwa wa Utandawazi ni anguko la asili yetu kwa kubeza UTANI WA
JADI,ambao ulikuwa silaha hata ya kurekebisha Vijana walio kuwa katika
dalili za kupotea kwa kuwarejesha katika Mstari wa tabia njema,tofauti
na leo ambapo Vijana si ajabu kupita nusu Uchi hata kwa wakwe zao
sembuse wazazi wake?
Kwa mwenendo uliopo na kasi ya utandawazi unazidi kuathiri mila zetu BURIANI UTANI WA JADI TANZANIA.
0 Response to "UTANDAWAZI UMEATHIRI MILA ZA BAADHI YA MAKABILA NCHINI."
Post a Comment