Habari za hivi Punde

VIJANA WANAOISHI MAISHA HATARISHI KUPANDA MITI MILLONI 10 BULYANHULU.

miti ovyo na wachimbaji wadogowadogo.


Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Kikundi hicho Mohamed Abdul wakati akitoa taarifa fupi kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyoitoa kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wadau ambao hujitokeza kuwasaidia vijana hao.
Katika hafla hiyo Abdul alisema Kikundi hicho maarufu kwa VIWAKAMAHAZA,tayari kimeotesha miche Elfu 10,ikiwa ni maandalizi ya upandaji miti katika eneo hilo la Bulyanhulu,itakayopandwa katika vijiji vya kata hiyo.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni Busindi,Busulwaangili,Namba  Tisa,Bushing’we,Lwabakanga pamoja na Kakola,ambapo ndio makao makuu ya kikundi hicho.
Hata hivo Mwenyekiti huyo alisema Kikundi hicho kina changamoto nyingi za kiuchumi kutokana na shughuli yake kuu ya kufanya  kazi za usafi katika mji wa Kakola,huku kikiwa hakuna vitendea kazi na vyanzo vya mapato vyenye uhakika.
Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana hao kuwa waaminifu katika kazi yao,kwani ndio njia pekee ya kupata wahisani watakaoweza kuwasaidia  ili waweze kujitania zaidi.
 

Mpesya kwa kuanzia aliwapa mashine moja ya kisasa ya kufyatua tofari za gharama nafuu ambayo alisema atawasaidia kuanzisha mradi wa ujenzi wa majengo mbalimbali ya Umma na watu binafsi.
Pamoja na msaada huo Mpesya aliwaonya vikali kuachana na siasa kwanza na kwa umri wao haujafikia kufanya hivyo kwakuwa hivi sasa wanapaswa kuimarisha uchumi kwanza kuliko kufanya siasa wakati hawana vipato na wengine kusotea hata mlo wa siku moja.

0 Response to "VIJANA WANAOISHI MAISHA HATARISHI KUPANDA MITI MILLONI 10 BULYANHULU."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.