Kutoka
Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga kuhusu
ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la Wananchi
Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo na shuhuda wa eneo hilo.
Msafara
huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye
camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo ya Mnolela kijijini
Lindi,kwa mujibu wa shuhuda ambaye ametoa taarifa hii kupitia kipindi
cha Power Breakfast kutoka Clouds Fm amesema ajali hiyo imeua wanajeshi 3
na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua kalala ndani.
Madhara
mengine yaliyotokana na ajali hii ni nyumba mbili kuharibika
vibaya,majeruhi wa ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa
Mtwara.
0 Response to "WANAJESHI WATATU WAFARIKI DUNIA KWA AJALI HUKO MTWARA."
Post a Comment