Habari za hivi Punde

WANAWAKE WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA NA RADI,WATOTO WAZIMIA -MBOGWE GEITA

WANAWAKE wawili wamefariki dunia huku watoto wawili pia wakipoteza  fahamu kwa muda wa masaa mawili mara baada ya kupigwa  na radi wakiwa nyumbani kwao huko katika kijiji cha Shinyanga  A kata ya Nyakafulu wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Watu hao ni Yunge Luhende (40) na Magreth Elias (18) waliofariki ambapo watoto wawili walipigwa na radi mnamo mnamo majira ya saa 4 asubuhi wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Temesto Sahani  alisema kuwa watoto waliopigwa na radi na kupoteza fahamu wote walikuwa wa marehemu Yunge Luhende  ikiwa walikuwa katika harakati za kukinga maji ya mvua iliyonyesha kwa kuanzia majira ya asubuhi saa  moja mpaka saa tano mfululizo ikiambatana na radi kali.
Pia sahani aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukinga maji kipindi cha mvua inayoambatana na radi huku akiwahasa wananchi kuacha kuchukulia tukio hilo kwa kuhusisha na imani za kishirikina.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Mussa Shabani alisema kuwa wakati mvua ikinyesha alisikia ghafla mayowe huku watu wakikimbia hovyo ,katika familia hiyo alikuta miili ya   wanawake hao ikiwa chini karibu na ukuta wa mlango huku watoto wakiwa wamezimia na kupoteza fahamu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani  Geita Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha kwa muda mrefu ikiwa imeambatana na radi huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kukaa kwenye kuta za nyumba au miti pindi mvua  inapokuwa inanyesha.

KARENY. Powered by Blogger.