Habari za hivi Punde

KIJANA MMOJA AUWAWA KWA WIZI WA NG'OMBE-KAHAMA MKOANI SHINYANGA
KIJANA  mmoja  aliyefahamika  kwa jina moja la Sabo mwenye umri wa miaka kati ya 30 hadi 34 ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe wawili katika kijiji cha Shininga kata ya Kilago wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

K amanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni ambapo mwanamme huyo mkazi wa Chibiso alipigwa na wananchi hao baada ya kumtuhumu kaiba ng’ombe wawili mali ya mtu ambaye hakufahamika jina wala makazi yake na thamani ya ng’ombe hao haijulikani.

Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako kuwabaini na kuwakamata wahusika wote wa mauaji hayo.
KARENY. Powered by Blogger.