MKURUGENZI wa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges ,Alexander Kazimil akitoa nasaha. |
MWITO
umetolewa kwa jamii kujenga hamasa ya upendo miongoni mwao itakayoibua ari ya
kutetea wanyonge sambamba na kuzingatia maadili ya dini hali itakayosaidia
kuliondoa Taifa katika matukio ya kufedhehesha kama ukatiri wa mauaji ya Albino
na vikongwe.
Mwito huo
ulitolewa juzi na Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Anderleck ya Mjini Kahama
Alexander Kazimiri katika mahafali ya 12 ya shule hiyo yaliofanyika mjini
Kahama huku wahitimu 158 wakihitimu kidato cha nne katika shule hiyo.
VIJANA wa shule ya Rocken Hill Academy walikuwepo katika mahafari hayo na kutoa burudani wa ngoma ya utamaduni wa Mtanzania. |
Mkurugenzi
huyo alilaani ukatiri huo huku akidai sababu kubwa ya ukatiri huo ni ufinyu wa
elimu hivyo kuomba jamii iwekeze zaidi katika sekta hiyo huku akiomba kila
Mtanzania kutimiza wajibu wake sambamba na walimu wakihakikisha wakiweka kipaumbele katika
mafundisho yao kupinga ukatiri huo hatua itakayosaidia kulinusuru Taifa na fedheha
hiyo.
Alisema
msisitizo ukiwekwa mashuleni ana uhakika vitendo hivyo ambavyo mbali na
kufedhehesha Taifa pia ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu vitatoweka huku
akisisitiza jamii kubadirika kwa sasa na kumwogopa Mungu kwani vitendo hivyo ni
vya kinyama na vinapaswa kukemewa na kila mtu ili viweze kutoweka kabisa.
MGENI rasmi katika Mahafari hayo,Afisa Mkuu wa Ugawaji Rasilimali kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania;Masozi Nyirenda,akitoa nasaha. |
“Taasisi
ya Anderlek tunalaani vitendo vya mauwaji ya albino vinavyofanywa na watu
wenye roho mbaya ,kwani ni kinyume na haki za binadamu, watu hawamuogopi Mungu
kwa kuweka kando vitabu vyake vitakataifu,badala yake wameweka mbele
mapanga,visu na mashoka kuwakata miguu na mikono hata kuwatoa uhai kaka na dada
zetu,”Alisema Kazimir
Hivyo
aliomba kila kada iwajibike kwa kuhakikisha inatokomeza mauaji hayo,kwa waumini
wa dini mbalimbali kushinda katika nyumba zao za ibada,askari polisi na vyombo
vya sheria navyo vitimize wajibu wao kwa wakati muafaka na kwa haki hali
itakayosaidia kutokomeza mauaji hayo ya watu wenye ulemavu wa ngozi na
vikongwe..
HII ni moja ya Burudani iliyotolewa katika Mahafari hayo. |
Aidha
aliiomba jamii kurudisha utamuduni wa zamani wa kujisomea vitabu
mbalimbali kwa muda mwingi ili kuweza kuweza kuongeza maarifa hali itakayo
saidia vijana wanahitimu elimu za juu kukabiliana na mataifa mengine katika
ushindani wa soko la Ajira Duniani.
Alisema
jamii nyingi za Kitanzania hazina utamaduni wa kujisomea Vitabu na hivyo
kuchangia kwa kiasi kikubwa kupitwa na mambo mengi yanayoendelea katika dunia
hii ya sasa na kuongeza kuwa wanafunzi wakati wakisubiri matokeo yao ni bora
wakawa wakijisomea vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa zaidi.
WAHITIMU hao nao walitoa burudani |
Mkurugenzi
huyo alidai kwa sasa Taifa limepoteza mwelekeo mkubwa hususani kwa vijana ambao
kwa kiasi kikubwa hawasikilizi hata vipindi vya Radio vyenye kuwaongezea maarifa
zaidi ya kukabiliana na maisha katika jamii ndio maana wamebakiwa kuwa
walalamikaji juu ya ugumu wa maisha.
Kwa upande
wake Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Afisa Mkuu Ugawaji Rasilimali
kutoka mamlaka ya Elimu Tanzania Masozi Nyirenda alisema kuwa kwa sasa
Wanafunzi wanatakiwa kuangalia masomo yatakayowajenga katika mbinu za kujiajiri
na si kusubiri kuajiriwa.
Masozi
aliwataka pia Wanafunzi wawapo majumbani wawe mabalozi wa kuweza kuripioti
matukio ya maovu yanayotendeka katika jamii kwani na wao ni mojawapo katika
sehemu ya jamii ambayo inatakiwa kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani.
0 Response to "WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UPENDO NA KUONDOKANA NA MAUAJI HARAMU YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO))"
Post a Comment