Habari za hivi Punde

WANAWAKE WAWILI MKOANI SHINYANGA WACHINJWA SHINGO ZAO NA WATU WASIFAHAMIKA



MKOA wa Shinyanga bado unaendelea kutikisa kwa mauaji yanayosaikiwa kusababishwa na imani za kishirikiana nchini baada ya wanawake wawili kutoka familia moja,kuuawa kikatili
baada ya kuchinjwa kwa panga na watu wasiofahamika wakati wakijiandaa kula chakula cha usiku.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Oktoba 14 mwaka huu saa mbili usiku katika kitongoji cha Nanzilo kijiji cha Ihugi,kata ya Lyamidati tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini.
Kamanda Kamugisha aliwataja  wanawake hao waliouawa  kikatili  kuwa ni Dilu Tungu(80) na mtoto wake Bunya Mihangwa(45),ambao ni wakazi wa kitongoji hicho.
Kamanda Kamugisha alisema wanawake hao wakiwa wanajiandaa kula chakula cha usiku na wanafamilia wenzao  ghafla walivamiwa na watu watatu wasiofahamika kisha kuanza kuwakata kwa panga sehemu mbalimbali za miili yao kabla ya kuitimisha unyama huo kwa  kuwachinja shingo hadi wakapoteza maisha.
Chanzo cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni imani za kishirikina kwani kuna mwanamme aitwaye Bwanya Mlyashimba(40) (ambaye anashikiliwa na polisi) mkazi wa Ihugi alikuwa akiwatuhumu marehemu hao kwamba walimroga yeye na kusababisha akose nguvu za kiume na kwamba walimroga 
 mama yake Hollo Mahangwa aliyefariki dunia mwaka 2013.

 Bwanya Mlyashimba anashikiliwa na jeshi la polisi,huku Jeshi hilo likiendelea na jitihada za kuwatia mbaroni  watuhumiwa wengine.

0 Response to "WANAWAKE WAWILI MKOANI SHINYANGA WACHINJWA SHINGO ZAO NA WATU WASIFAHAMIKA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.