Habari za hivi Punde

TEKNOLOJIA YA KISASA IMEWEZA KUATHIRI UPATIKANAJI WA WAHALIFU

IMEELEZWA kuwa mfumo mpya wa utunzaji wa siri za mtumiaji wa simu uliowekwa na makampuni ya Apple na Google unatengeneza “shimo jeusi katika utekelezaji wa sheria ya upelelezi” ambapo itapelekea uhalifu wa kisasa kushindwa kubainika kwa urahisi.

 
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa shirika la upelelezi Marekani (FBI) James Comey, alisema kutokana na kubainika hali hiyo kuibuka mvutano ambao umedumu kwa miaka mingi kuhusiana na kupanua mwanya wa sheria ya upelelezi ambao utaipa mahakama mamlaka ya kutoa amri kwa makampuni husika kutoa taarifa za siri za mtumiaji wa vifaa hivyo vipya.
Comey amesema sheria ya upelelezi haikuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia, huku akiongeza kuwa hali hiyo inatishia kukua kwa tatizo la usalama wa jamii, huku akiita kitendo cha usiri katika vifaa hivyo ni ‘kiza endelevu’, kwa kuwa wale wenye jukumu la usalama wa watu hawana fursa ya kupata ushahidi utakaosaidia kumshtaki mhalifu na pia kuzuia ugaidi.
Comey amekiri kutambua malalamiko yaliyotokana na kitendo cha kuvujishwa kwa taarifa za siri za idara ya usalama wa taifa la Marekani (NSA), na aliyekuwa mfanyakazi wake wa zamani, Edward Snowden.
Aidha amesema uwezo wa serikali katika kupeleleza taarifa hizo ni wa kawaida, lakini kile ambacho kimekuwa kikielezwa kuhusiana na upelelezi huo ‘kimezidishwa chumvi’
Makampuni ya Apple na Google yameanza kuuza mfumo mpya wa uendeshaji simu za mkononi (operating system) ambao wamenadi kuwa mfumo huo unaficha namna yoyote ya upelelezi wa taarifa za mtumiaji wa kifaa hicho, na hata amri ya mahakama kwa kampuni hizo haitotoa ruhusa kwa sheria ya upelelezi kuingilia taarifa binafsi za mmiliki, isipokuwa zile zilizowekwa katika mitandao na mtumiaji husika.
Comney amesema taarifa zinazowekwa na watumiaji wa simu na vifaa mbali mbali katika mitandao haziwezi kumbainisha mhalifu hivyo sheria haiwezi kuishia kutegemea ushahidi wa taarifa za mhalifu kupitia mitandao.
Aidha amesema kuwa watu wengi wanaokiuka sheria na wahalifu wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali kuhakikisha taarifa zao hazipatikani, hivyo matumizi ya vifaa hivi huenda ikawa kivuli cha kuficha siri za uhalifu.
KARENY. Powered by Blogger.