Tanzania imetuma timu ya madaktari bingwa watano wa magonjwa ya mlipuko
ikwemo Ebola katika nchi ya Siera Leoni watakaoenda kusaidia kutoa
huduma kwa wagonjwa wa ugonjwa huo hatari wakata taifa hilo na mataifa
mengine ikiwemo Laiberia yakiendelea kukubwa na ugonjwa huo ikiwa ni
mkakati wa nchi katika kushiriki katika nguvu ya mataifa ya umoja wa
Afrika kudhibiti ugonjwa huo.
Akitoa taarifa hiyo katika wizara ya afya nchini mganga mkuu wa
serikali Dk. Donani mmbando amesema timu ya madaktari hao itaondoka
nchini tarehe 8 octoba mwaka huu kwenda kushirikiana na madaktari
wengine katika nchi ya Liberia na kuongeza kuwa Tanzania inatambua
tishio la ugonjwa huo na ipo tayari kuendelea kutoa msaada katika
mataifa yaliyoathirika ili kuhakikisha wagonjwa wa ugonjwa huo wanapona
kupunguza kasi ya maambukizi.
Dk. Mmbando licha ya kukiri jithada zilizokwisha kuchukuliwa na
serikali katika kujiandaa kupambana na ugonjwa huo amekiri bado nchi
haina maabara daraja la tatu yenye uwezo wa kugundua mgonjwa mwenye
ugonjwa huo na mpaka sasa kinachoweza kufanyika nchini ni kupima joto la
mwili pekee na kubaini kuna hatua za kuboresha maabara yenye darala la
kukaribia la tatu iliyopo mkoani Mbeya.
Baadhi ya madaktari hao wanaoondoka nchini leo licha ya kukiri
kuogopa ugonjwa huo wamesema hatua ya maambukizi iliyofikiwa hivi sasa
ni lazma kila daktari mwenye uwezo wa kutibu ugonjwa huo aamke na kutoa
mchango wake katika kudhibiti maambukizi mapya kwani ugonjwa huo hatari
hauchagua mipaka na unaweza hata kuingia nchini Tanzania.
0 Response to "TANZANIA YAENDA KUTIBU UGONJWA WA EBOLA AFRIKA MAGHARIBI"
Post a Comment