Habari za hivi Punde

MENO YA TEMBO YAKAMATWA HUKU WATU TISA WAKISHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

WATU wadhanwao ni  majangili katika pori la akiba Maswa waliofanya tukio la  kutungua
helkopita ya kampuni ya Mwimba Holding Limited na kusababisha kifo cha
Rubani,  Rodgers Charvis  raia wa Uingeleza ambaye alikuwa
akitekelezamajikumu yake jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata
wahusika 9 pamoja na bunduki 29  ikiwemo  meno ya tembo matatu.

Akiongea  jana na waandishi wa habari mkoani Simiyu, Kamanda wa polisi
mkoani hapa Lazaro Mambosasa alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 9 ambao walihusika na tukio la kuangusha
helkopita pamoja na kusababisha kifo cha Rubani wa ndege hiyo.

WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MAHAKAMA ZA MWANZO




 WATUMISHI  wa idara ya mahakama mkoani Shinyanga wametolewa hofu ya kuhakikisha wananchi  wanashirikishwa ili kuweza  kuboresha miundombinu ya majengo  kama wafanyavyo kwenye sekta zingine.

Hayo yamesemwa   na mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga   kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyka kwenye viwanja vya mahaka mkazi wilaya nakuhusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA ATAKA WANANCHI KUFAHAMU TARATIBU NA SHERIA DHIDI YA VYOMBO VYENYE DHAMANA


MKUU wa wilaya ya Shinyanga  Josephine Matiro  ametoa wito kwa wananchi  kushiriki utolewaji wa elimu  katika vyombo vinavyosimamia haki na sheria  ili kuweza kujua pindi haki inapotendeka nakuondoa manung’uniko yanayotokea mara kwa mara katika vyombo hivyo.
KARENY. Powered by Blogger.