Habari za hivi Punde

REDIO ZA JAMII NCHINI KUPIGWA DARASA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.

REDIO ZA JAMII NCHINI  KUPIGWA DARASA NA  MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.
DSC_0009
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.

Beatrice alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.

Alisema uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
DSC_0081
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma.

Naye Afisa mfawidhi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Ludovick Ringia akizungumzia sheria mbili za vyama vya siasa alisema kwamba ni wajibu wao kuwaeleza wananchi kuhusu maadili na kanuni katika sheria zinazogusa ukuzaji wa amani katika duru za siasa na demokrasia.
Alisema mradi huo wa kuelimisha wananchi ambao unafanyika kwa udhamini wa Unesco kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ni moja ya njia za kufanikisha amani katika kipindi chote kuanzia uchaguzi wa mwisho hadi mwingine.
Alisema wanatumia redio za jamii kwa kuwa redio za kibiashara zimekuwa kikwazo hasa bajeti inapouma kidogo.
Alisema mradi huo ambao unafanyika kwa mwaka mmoja ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo za kuliwezesha taifa kuendelea kuwa na utulivu.
DSC_0073
fisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia), akielezea uwezo wa redio za jamii zinavyoweza kufikia jamii kubwa zaidi nchini wakati ujumbe kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ulipofanya mazungumzo na Wenyeviti wa Bodi na Mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na shirika maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO iliyofanyika kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
Wenyeviti wa bodi na mameneja hao katika warsha hiyo walielemishwa uboreshaji wa masoko na umuhimu wa redio za jamii juu ya matumizi ya Tehama kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na kushirikisha zaidi wananchi.
Aidha Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Al Amin Yusuph akizungumzia mafunzo hayo alisema kwamba mradi huo umekuja wakati muafaka ili kutoa elimu kwa umma, kwani kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa takribani asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini wanasikiliza redio huku asilimia 5 tu ndio wanaangalia runinga.

DSC_0013
Meza kuu: Kutoka kushoto ni Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko, Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Mwenyekiti wa Warsha hiyo kutoka Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara, Bw.Baraka Ole Maika (katikati), Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia).
Uelewa huo upo katika sheria za uchaguzi, gharama na kuona wajibu wao wa kumsaidia Msajili wa Vyama vya Siasa kukabiliana na mazingira hatarishi ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Alisema ni kazi ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria ya vyama namba tano ya mwaka 1992 ya kusajili vyama na kuviangalia na ile ya namba sita ya mnwaka 2010 ambayo inagusia gharama za uchaguzi.
Mratibu huiyo amesema kwamba timu kutoka Ofisi ya Msajili itafika kwenye redio hizo za jamii na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wao katika siasa na kuimariuka kwa demokrasia.
Aidha elimu hiyo inatarajiwa kuwasaidia wananchi kutambua kwamba wana wajibu katika kuhakikisha kwamba menejimenti za uchaguzi zinawajibika pamoja na muuingiliano wake ili kuwa na michakato salama ya cuhaguzi na uchaguzi wenyewe.
DSC_0119
Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia) akielezea ufanyaji kazi wa sheria mbili za vyama vya siasa kwa wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini wakati wa warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na SIDA na kuratibu na UNESCO ambayo imefanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0034
Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko akiwasilimia wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini (hawapo pichani).
DSC_0135
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akihoji swali kwa ujumbe uliotoka kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.
DSC_0126

BAADHI YA WANANCHI PEMBA WAGAWANA NYAMA YA NYANGUMI KWAAJILI YA KITOWEO.

 


Wafanyakazi wa Uvuvi pemba wakimpima Nyangumi aliyeonekana Pemba akiwa ameanguka ufukwe wa bahari wa shamiani.


Wananchi wakikata minufo ya Nyangumi aliyeangukia katika ufukwe wa bahari ya Pemba maeneo ya shamiani, kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika harakati hizo.

SABABU YA KUFARIKI KWA WATOTO MAPACHA HOSPITALI YA MKOA NESI AWAJIBIKA KWA UTENDAJI MBOVU.

Mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga usiku huu,nje ya wodi namba 8 ya wazazi wakifurahia waandishi kufika eneo la tukio,ambapo jioni hii kumetokea sereka la aina yake baada ya nesi mmoja(Jina tunalo) ambaye amedaiwa kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha,inadaiwa kuwa mama mjamzito kafikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua lakini nesi aliyekuwepo alikuwa bize na simu ya mkononi bila kumjali/kumpatia huduma yoyote pamoja na kuombwa na ndugu zake na mama huyo kuwa tayari alikuwa ameanza kupush matokeo yake watoto wote wakafariki dunia.Inaelezwa kuwa nesi alikuwa yuko bize na simu ya mkononi akichat

Bi  Mwanaisha Juma mkazi wa Mshikamano mjini Shinyanga Mama mzazi wa mama aliyefikishwa hospitalini hapo,akizungumza na waandishi wa habari walifika eneo la tukio ambaye alisema amemfikisha mwanaye  Zena Pius kujifungua  tangu saa 6 na nusu mchana leo na (Uchungu)dalili za kujifungua zimeanza saa 7 na ilipofika saa 10 wakiwa hospitalini hapo wodi namba 8 alianza kupush wakaomba msaada kwa manesi waliokuwa zamu lakini hakuna aliyejali matokeo yake watoto wakafariki dunia saa 10 na nusu.Kwa mujibu wa mama huyo nesi aliyewa zamu alikuwa bize na simu takribani nusu saa hadi akaja nesi mwingine kutoa msaada 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la aina yake akizungumza na waandishi wa habari usiku huu

Waandishi wa habari wakiwa kazini eneo la hospitali ya mkoa wa Shinyanga usiku huu

Waandishi wa habari wakiwa nje ya ofisi ya mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa ,ili kujua undani wa tukio hilo,ingawa hata  hivyo baada ya kumsubiri muda wa takribani nusu saa akizungumza na nesi huyo ofisini kwake,nesi huyo alitoroshwa na baada ya kuingia ofisini,aliwaambia waandishi wa habari kuwa  yeye siyo msemaji,msemaji ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt Ntuli Kapologwe na kwamba taarifa kamili itatolewa kesho asubuhi kwani bado wanafuatilia undani wa tukio hilo

Nesi anayetuhumiwa kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha akitoroshwa hospitalini akiwa amejifunika nguo ili waandishi wasimpige picha
Gari lililotumika kumtorosha mtuhumiwa,siti ya nyuma akiwa amejifunika nguo

Picha zote na Mwandishi Maalum wa Malunde1 blog

UNESCO YAWAFUA WATENDAJI WA REDIO ZA JAMII NCHINI.

UNESCO YAWAFUA WATENDAJI WA REDIO ZA  JAMII  NCHINI.
DSC_0014
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama kwa mameneja na waandishi wa habari takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
Na Mwandishi wetu, Sengerema
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema litaendelea kusaidia kuimarika kwa redio za jamii nchini kwa kuwa ndio nyenzo muhimu za maendeleo ya wananchi kwa kuwapa sauti katika huduma na shughuli zao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja na watendaji takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, mafunzo yanayofanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema FM.
Katika mafunzo hayo watendaji hao watafunzwa masuala ya Tehama na utafutaji wa soko kwa lengo la kufanya redio hizo kuwa endelevu na kujiendesha zenyewe kwa kuweza kutekeleza miradi yake na kuendelea kushirikiana na wananchi.
Mafunzo hayo ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu wa kuwezesha redio za jamii nchini unaoendeshwa na UNESCO baada ya redio hizo nyingi kusaidiwa kuanzishwa katika miaka ya karibuni.
DSC_0045
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akizungumza na Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio tisa za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na matumizi ya Tehama yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Kushoto mgeni rasmi Ofisa mdhani kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed.
Kwa mujbu wa Yusuph mradi wa SIDA ambao umekuwa ukitekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu umeshughulika na uboreshaji wa redio hizo ili kuzipatia uwiano na pia kuziwezesha kutumia Tehama kuhabarisha wananchi pia kutokana na mafanikio yaliyopatikana mradi huo utaendelea kwa miaka mingine mitatu.
Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana kwa ushirikiano wa Redio za jamii pamoja na shirika hilo hali iliyofanya kuyavuta mataifa mengine kuchangia kwa ajili ya kuendelea kuzijengea uwezo redio za jamii kupitia shirika hilo.
Ameongeza kuwa kufanikiwa kwa redio za jamii nchini Tanzania katika mradi huu wa SIDA kumefanya mashirika mengi yanayotaka kufanyakazi na wananchi wa kawaida kukimbilia UNESCO kutambua redio za jamii ambazo zinaweza kufanyakazi nayo.
Mradi huo wa Tehama unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO ni sehemu ya mradi wa UNESCO katika nchi saba za Afrika , Tanzania ikiwamo.
DSC_0036
Baadhi ya Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii wakimsikiliza Bw. Al Amin Yusuph kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Katika mafunzo hayo yanayofanyika mjini Sengerema, elimu inatolewa kwa wakuu wa vituo na waandishi wa habari kutoka redio Micheweni FM, Orkonerei FM, Pambazuko FM, Mtegani FM, Kahama FM, Redio FM, Kyela FM, Fadeco Radio na Pangani FM.
"Kuna mambo mengi yamefanikiwa.. kikubwa zaidi kumpa nafasi mwananchi kujieleza na kueleza matumaini yake.." alisema Yusuph ambapo aliongeza kwamba kutokana na mradi huo kufanikiwa zipo nchi na mashirika ambayo yapo tayari kuchangia uimarishaji wa redio za jamii nchini.Hakuzitaja nchi hizo
Alisema kutokana na mafanikio yaliyopo ya redio hizo kuwa karibu na jamii, SIDA kwa kushirikiana na UNESCO wametengeneza programu hiyo ili kuwezesha kuwepo kwa matumizi ya mtandao katika kukusanya habari, kuziboresha na kuzitumia kwa manufaa ya wananchi.
DSC_0005
DSC_0060
Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed, akitoa baraka zake tayari kuanza mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama mameneja na waandishi wa habari takribani 60 kutoka redio za jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema kutekelezwa kwa mradi huo ni utekelezaji wa azimio la Windhoek la mwaka 1991 linalohimiza matumizi ya redio jamii katika kuboresha maisha ya wananchi kutokana na kuonekana dhahiri kwamba wananchi wanapokuwa na nafasi ya kujieleza wanaweza kufanya makubwa zaidi.
Akifungua mafunzo hayo Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi redio jamii Micheweni, Ali Mohamed aliwataka mameneja na watendaji wa radio hizo kutekeleza ushauri wa UNESCO ikiwa na pamoja na kutekeleza maagizo ya utengenezaji wa vipindi vya vijana ili kupata nafasi ya kushindania nafasi moja ya upendeleo kwenda Paris , Ufaransa mwakani kwa tamasha la redio za jamii.
Aidha aliwataka watendaji kuwa makini katika kazi zao kutokana na serikali kuweka mazingira sahihi ya uendeshaji wa radio hizo kwa manufaa ya umma.
DSC_0092
Mkufunzi wa darasa la mameneja wa redio mbalimbali za jamii Mkurugenzi Mtendaji wa ASMET, Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya siku tano ya namna ya kuingiza kipato pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya kuendeleza vituo vyao yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0079
Baadhi ya mameneja wa redio mbalimbali za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya masoko na ujasiriamali yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0120
Meneja wa kituo cha redio Orkonerei FM, Bw. Lucas Kariongi akihoji swali kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
DSC_0101
Mhasibu wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre, Bw. George Tumbo akiongaza washiriki wenzake katika kazi za vikundi wakati wa mafunzo hayo.
DSC_0171
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mafunzo ya matumizi ya Tehama kuwajengea uwezo wa kuweka kumbukumbu za vipindi na kukusanya vyanzo vya habari kwa kutumia "Tablet" kwa waandishi wa habari wa redio mbalimbali za jamii yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na shirika la UNESCO yanayoendelea kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0156
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya matumizi ya "TABLET" katika kuhifadhi na kuandaa habari kwa kutumia kifaa hicho.
DSC_0142
Pichani juu na chini ni washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya "TABLET".
DSC_0136

MAANDAMANO CHADEMA YAZIMWA GHAFLA,POLISI WATANDA KUANZIA ALFAJIRI



Hivi ndivyo jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limejipanga kukabiliana na maandamano yaliyotangazwa na Chadema jana ya kupinga bunge la katiba ambayo yalitarajiwa kufanyika kuanzia leo saa mbili asubuhi lakini mpaka sasa hakuna kiongozi wa chama hicho aliyejitokeza,hata ofisi ya Chadema imefungwa tangu asubuhi.
 FFU wakiwa mtaani kukabiliana na waandamanaji kama watajitokeza leo.

KATIBU WA CCM TAIFA KINANA ASAFISHA SHAMBA LA UMOJA WA VIJANA MJINI KIBAHA ABAINI CHANGAMOTO HOSPITALI YA TUMBI

KATIBU WA  CCM TAIFA KINANA ASAFISHA SHAMBA LA UMOJA WA VIJANA MJINI KIBAHA ABAINI CHANGAMOTO HOSPITALI YA TUMBI
8
Add caption
Katibu mkuu pia anahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuimarisha chama, Katika msafara huo Kinana anaogozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. Kero kubwa iliyojitokeza katika ziara hiyo ni pale Mkurugenzi wa huduma za Afya katika hospitali ya Tumbi Dr. Peter Dattan aliposema Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliahidi kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo(ICU) Lakini ahadi hiyo haijatekelezwa yapata miaka mitatu sasa, Pamoja na kwamba hospitali ya Tumbi Kibaha inapokea majeruhi wengi na wanahitaji tiba maalum kutokana na majeraha mbalimbali yanayosababishwa na majeruhi wa  na ajali, Hospitali ya teule ya Tumbi inapokea asilimia 80% ya majeruhi wa ajali.
2Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka akitoa maelezo ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha kwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo ambali ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha inajegwa mjini Kibaha6Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akipanda mti katika jengo la ofisi mpya ya CCM wilaya ya Kibaha inayojengwa.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapongeza watoto wa chipukizi baada ya kuimba ngonjera yao mbele yake. (picha na kikosi kazi cha africanmishe.blogspot.com)

CHUO KIKUU HURIA KITUO KIPYA CHA SHINYANGA KIMEZINDULIWA,ONGEZEKO LA WADAHILI SERIKALI KUFANYA MIKAKATI.


CHUO kikuu huria huria jana kimezindua  kituo kipya na majengo yake  ambapo sherehe za uzinduzi huo zilifanyika mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Jenista Mhagama   ambaye ni naibu waziri wa elimu na ufundi  pia mbunge wa jimbo na Peramilo-Songea,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali  wa mkoa wa   Shinyanga na Simiyu,katika uzinduzi huo kulikuwepo na wahitimu  wa chuo hicho akiwemo mkuu wa mkoa  wa Shinyanga Ally Rufunga na kutunikiwa cheti,hivyo mgeni rasmi huyo alifutahishwa na chuo hicho  kwa kuweza kudahili jumla ya wanafunzi 95,000 nchini wanaochukua masomo kwa mfumo wa masafa marefu huku akiwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuchukua fursa  iliyopo na ukaribu wa chuo tofauti na mikoa mingine  na kuwapunguzia gharama ya safari kutafuta elimu hiyo.



Baadhi ya wanachuo wanaoendelea na masomo na wale wanao maliza wakisikiliza kwa umakini mkubwa maneno yaliyokuwa yakitolewa na mgeni rasmi ikiwemo viongozi wa chuo hicho.


Makamu wa chuo hicho Pro Tolly  Mbwette  akieleza wageni waalikwa walio kwenye meza kuu na wananchuo kuwa  mfumo wa kupata elimu kwa masafa marefu  umeweza kudahili wanachuo zaidi ya 90,000 nchini   huku ikiwapa fursa ya kuendelea na shughuli zao,lakini kumekuwepo na changamoto katika mfumo huo wa kupotza udahili  na chuo kuamua kuunda uongozi  utakao toa ushauri ,hivyo idadi ya wadahili imezidi kuongezeka  na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Shinyanga  kwenda na wakati kwa kupata mafunzo  ya TEHAMA ni muhimu  ili kuendana na utandawazi.


Wakati wa utambulisho ukiendelea  mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose  Nyamubi na mkuu wa wilaya ya Kishapu Wislon Nkhambaku wakiteta jambo kwa kunong'ona wakiwa meza kuu.


Kaimu mkurugenzi wa kituo cha chuo kikuu huria mkoani Shinyanga Agatha Mgogo akisoma taarifa ya chuo hicho mbele ya wageni waalikwa  ambapo alisema kuwa changamoto  ya chuo hicho ni idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaojitokeza kujiunga na chuo hicho hukua akieleza chuo hicho kilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2000   na jumla ya wanachuo 2168 na waliohai ni 227, hivyo mwaka 2010 kilianzisha  mafunzo ya komputa  na kufanikiwa kuhitimu wanachuo 884 na mpaka sasa  jumla ya wahitimu 334 kwa kozi mbalimbali,pia  ujenzi wa kituo hicho kipya umegahrimu jumla ya shilingi millioni 143.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose  Nyamubi akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu waliofika katika uzinduzi huo.

Mhe.Jenista Mhagama  baada ya kukaribishwa kutoa hotuba yake alikipongeza chuo hicho kwa kupiga hatua kubwa  na kueleza serikali haina budi kukisaidia,alisema vyuo vikuu vya serikali na binafsi  vinavyosimamiwa na TCU vimedahili jumla ya wanafunzi 52,538 ukienda kwenye mfumo rasmi  unaodahiliwa na  TCUni wanafunzi 38,817 ambapo waliokwenye mfumo wa elimu ya ufundi (VETA) kwa kudahili wanafunzi 8656 na vyuo ambavyo haviko  mfumo rasmi wa TCU vimedahili jumla ya wanafunzi 5265  na kuwataka wananchi kujifunza  mifumo iliyopo ili kuweza kubadilisha maisha  na kuwa bora kama zilivyofanikiwa nchi nchingine  kama China na India.


Wanachuo wakitumbuiza kwa nyimbo na mashairi mbele ya mgeni rasmi.

Add caption


Mgeni rasmi akikata utepe  katika ufunguzi wa jengo jipya la chuo kikuu huria lililopo maeneo ya Mwasele kata ya Kambatage manispaa ya Shinyanga.


Mgeni rasmi ambaye ni waziri wa elimu na ufundi mara baada ya kuingia katika uwanja wa jengo hilo huku akiwa na uongozi wa chuo hicho sanajri na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

KARENY. Powered by Blogger.