Habari za hivi Punde

BASI LA SIMBA MTOTO LIMEGONGANA USO KWA USO NA LORI ENEO LA MTO WAMI.

BASI  LA SIMBA MTOTO  LIMEGONGANA USO KWA USO  NA LORI ENEO LA MTO WAMI.
Ajali Bus la Simba Mtoto Lagongana Uso kwa Uso na Lori, Tunaomba Radhi kwa Picha hizi
Hili ndio gari lililopata ajali hivi punde.

Habari Zilizotufikia hivi punde zinaeleza kutokea kwa ajali ya bus la Simba mtoto na lori zimegongana uso kwa uso eneo la Wami ila taarifa za a hivi ali zimebainisha kuwa dereva wa lori amefariki papo hapo huku abiria wa simba mtoto baadhi yao kupatwa na majeruhi-Picha na Frank msaki

Taarifa kamili Tutakuletea ....

KIKAO CHA KAMATI YA MICHEZO MKOA WA TANGA WATAKA MICHEZO IPEWE KIPAUMBELE KWA VIJANA.

Kikao cha kamati ya mkoa wa tanga cha mwaka 2014

 Afisa michezo mkoa wa tanga,Digna Tesha akitoa ufafanuzi kwenye kikao cha kamati ya michezo mkoa wa tanga.
 Wajumbe waliohudhulia mkutano wa kujadili hali ya michezo mkoa wa tanga.


 Baadhi ya wajumbe wakichangia juu ya vyama ambavyo havijafika wilayani. 
 Wajumbe wakimsikiliza afisa michezo wa mkoa wa tanga ambaye hayuko pichani.
Afisa michezo wa wilaya ya pangani akichangia kwenye kikao.cha michezo mkoa wa tanga.

KUKOSEKANA ELIMU YA UZAZI WA MPANGO KUMESABABISHA MWANAMKE KUTELEKEZWA MSITUNI NA MUMEWE .


Mama mmoja mkazi Mabwepande wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam amevamia kituo cha ITV akiwa na watoto mapacha sita kulalamikia kuishi maisha ya tabu na watoto wadogo baada ya kutelekezwa na mumewe kwa madai ya kuzaa kupita kiasi.

Akizungumzia maisha yake mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Salome Paulo Mhando mkazi wa Mabwepande, amesema mume wake amemtelekeza na kumuacha na watoto mapacha sita kwa madai ya kuzaa watoto mapacha kila anaposhika ujauzito na kusababisha familia kuwa kubwa kupita kiasi huku akijua wazi kuwa kupata mapacha ni mipango ya mungu.
Kutokana na kuishi katika maisha ya mateso ameomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia ili aweze kupata mavazi, chakula na matibabu ya watoto huku akisisitiza kusaidiwa kupata mtaji wa kufanya biashara ya mkaa hivyo yeyote atakayeguswa afikishe msaada wake katika kituo cha ITV Mikocheni jijini Dar es salaam au atume mchango wake kupitia Tigo pesa 0715 358535.

MWILI WA BINADAMU ULIOKAA MOCHWARI KWA ZAIDI YA SIKU 50 HATIMAYE UMEZIKWA KIMYAKIMYA -MKOA WA KILIMANJARO MOSHI


Hatimaye mwili wa Rosemary Marandu uliohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa siku 53 umezikwa huku maziko hayo yakigubikwa na utata na kuhudhuriwa na wanaume sita.
 
Mazishi hayo yalifanyika juzi saa 10:30 jioni katika Makaburi ya Karanga mjini hapa na hakuna aliyehudhuria kati ya baba wala mama wa marehemu.

Taarifa za kufanyika kwa siri kwa maziko hayo zililifikia gazeti hili saa 10:40 jioni na waandishi walipofika makaburini, waliambulia kukuta mishumaa iliyokuwa ikiwaka ikiwa imewekwa juu ya kaburi na hakukuwa na mtu hata mmoja.

Mashuhuda wa tukio hilo, waliozungumza na gazeti hili, walidai kuwa waliyaona magari mawili yakiingia makaburini hapo, moja likiwa limebeba maiti na kushuhudia watu sita wakishuka katika magari hayo ambao waliuzika mwili huo.

Hata hivyo, bado kuna utata kuhusu nani hasa aliyefanya maziko hayo baada ya baba wa marehemu kudai ni mtoto wa marehemu aitwaye Witness Marandu na mkewe Felicia akikanusha.

Maziko hayo yamefanyika ‘chapchap’ wakati marafiki wa karibu na Marandu walipokuwa katika jitihada za mwisho za kumshawishi aukabidhi kwa mama wa marehemu juzi mchana ili auzike.


Kauli ya Baba wa Marehemu

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi usiku kutoka wilayani Rombo, baba wa Rosemary, Flavian Marandu alisema mtoto wa marehemu aliyemtaja kwa jina la Witness Marandu (17), ndiye aliyeuchukua mwili huo na kwenda kuuzika.

Marandu alisema mtoto huyo alimfuata akiwa amefuatana na ndugu wengine ambao hakuwataja akiomba apewe mwili wa mama yake ili akauzike.

Alidai kuwa awali aliwapa uhuru wa kuchagua sehemu ya kwenda kuzika katika moja ya mashamba yake yaliyoko Kitirima Kingachi wilayani Rombo au katika makaburi ya umma watakayoona yanafaa.
Marandu alisema baadaye akiwa amepumzika akiugulia maumivu ya kutoa jino, wanaukoo hao pamoja na mtoto wa marehemu walimpigia simu na kumshukuru kwamba wameshazika salama.

Mgogoro huo wa kugombea maiti ni wa pili kuhusisha ukoo wa akina Marandu, miaka takriban 10 iliyopita, maiti nyingine ya mwanaukoo huo ilikaa mochwari kwa zaidi ya siku 90 baada ya kutokea mgogoro unaofanana na huo.
Mama ageuka mbogo
Hata hivyo Felicia Nkya ambaye ni mama mzazi wa marehemu aliliambia gazeti hili si kweli kuwa mjukuu wake (Witness) ndiye aliyeuchukua mwili huo na kwenda kuuzika.
Alisema madai ya mumewe kuwa mjukuu huyo alimfuata juzi kuomba akauzike mwili huo hayana ukweli kwani mpaka siku hiyo, Witness alikuwa yuko shuleni mkoani Mbeya.

MKAZI WA KIJIJI CHA MWAKITOLYO WILAYANI SHINYANGA AVAMIWA USIKU NA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE.

Mkazi wa kijiji na kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga  Mageni Buhimili(54)  ameuawa kwa kukatwa panga kichwani,mikononi na tumboni wakati akila chakula cha usiku nyumbani kwake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Oktoba 26 mwaka huu saa moja na nusu usiku.

RAIS WA ZAMBIA MICHAEL SATA AFARIKI DUNIA



HATIMAYE baada ya kuibuka uvumi siku ya Jumanne kuamkia Jumatano juu ya kufariki kwa rais wa Zambia Michael Sata, Serikali ya nchi hiyo imethibitisha kifo chake.

Kwa mujibu wa katibu wa baraza la mawaziri, Roland Msiska amethibitisha kifo hicho  cha Sata {77}  kilichotokea baada ya rasi huyo kusafirii kuelekea jijini London Uingereza juma moja lililopita kwaajii ya kupata matibabu.

MNIGERIA ARUKA UKUTA WA IKULU YA MAREKANI MARA MBILI SASA APATA MATATIZO.

MNIGERIA ARUKA UKUTA WA IKULU YA MAREKANI MARA MBILI SASA APATA MATATIZO.

Adesanya 
Moja ya taarifa zilizochukua nafasi  wiki iliyopita ni kuhusiana na tukio la mtu mmoja kuruka ukuta wa ikulu ya Marekani, na baadaye kukamatwa baada ya kushambuliwa na mbwa kabla ya kutiwa nguvuni na walinzi wa ikulu hiyo, Secret Service.


Habari zinasema hii si mara ya kwanza kwa Mnigeria Dominica Adesanya (23) kuruka ukuta wa White House, na safari hii baada ya kumfikisha mahakamani imebainika kuwa ana tatizo la akili hivyo hawezi kushitakiwa akiwa na hali hiyo.
Daily Mail imeripoti kuwa baada ya mahakama kuthibitisha vipimo kutoka hospitali kuwa ana tatizo hilo, mahakama iliamuru awekwe chini ya ulinzi huku akipata matibabu ya ugonjwa huo mpaka Desemba 22 kesi yake itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Adesanya ametolewa mahakamani hapo akipiga kelele za kuomba msaada huku akilaumu kitendo cha kukamatwa kwake.
Hii ni mara ya pili kwa jamaa huyo kuruka ukuta wa White House, ambapo mara ya kwanza Adesanya ambaye ana asili ya Nigeria kufanya hivyo ilikuwa Julai 27 majira ya saa 4 usiku mwaka huu, na kurudia tena Oktoba 23 majira ya saa 1 jioni

MABOMU MANNE YA KIVITA YAMEKAMATWA YAKIWA YAMEHIFADHIWA ARDHINI HUKO MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR

MABOMU MANNE YA KIVITA YAMEKAMATWA YAKIWA  YAMEHIFADHIWA ARDHINI HUKO  MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR


  Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema mabomu hayo yameingizwa Zanzibar kupitia mtandao maalumu ambao umekuwa ukifanya vitendo vya uhalifu kwa kutumia mabomu hayo

TIMU YA YANGA YAZIDI KUNG'ARA NI BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI MNONO WA MABAO 3-0 DHIDI YA STEND UNITED YA MKOA WA SHINYANGA

TIMU YA YANGA YAZIDI KUNG'ARA NI BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI MNONO WA MABAO 3-0 DHIDI YA STEND UNITED YA MKOA WA SHINYANGA

http://images.supersport.com/2013/5/Yanga-celebrate-300.jpg 
Bunda la mkosi limeendelea kuiandama Simba baada ya kulazimishwa tena sare ya bao moja kwa moja na maafande wa Prisons katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wakati mahasimu wao Yanga wakipata ushindi mnnono wa 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.

AJALI YA HIACE -MOSHI, MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU


Hii ndiyo Hiace inavyoonekana mara baada ya kupata ajali

Wananchi wakienda kushuhudia ajali hiyo na kutoa msaada kwa majeruhi.
Wananchi wakiangalia Hiace hiyo iliyopata ajaliMajeruhi wa ajali hiyo wakiwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidiWananchi wakiuangalia mwili wa aliyefariki katika ajali hiyo (uliofunikwa kwa kitenge katikati ya barabara)Ajali mbaya ya gari imetokea hii leo katika eneo la KNCU barabara ya Kibosho Kirima Moshi Kilimanjaro, baada ya gari la abiria (hiace) kupata ajali huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi
Kwa mujibu wa ripota wa eddy blog aliyefika eneo hilo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni na abiria kadhaa wamejeruhiwa na kukumbizwa hospitali kwa matibabu zaidi huku abiria mmoja akihisiwa kufariki dunia katika ajali hiyo
Hizi ni taarifa za awali na eddy blog inaendelea kufuatilia taarifa za ajali hiyo ili uzipate kwa uhakika, endelea kuwa nasi mara mara
Picha na Thade Expensive wa eddy blog, Moshi

BOT KUTOA NOTI YA SHILINGI 1000 NI BAADA YA MALALAMIKO KUTOKA KWENYE FAMILIA YA HAYATI BABA WA TAIFA.

BOT KUTOA  NOTI YA SHILINGI 1000  NI BAADA   YA  MALALAMIKO KUTOKA  KWENYE FAMILIA YA HAYATI BABA WA TAIFA.


Shillingi elfu 1
Kumbukumbu zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi kama hazipo sawa, ichukue hiyo.

Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania,
Marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo mkurugenzi wa huduma za kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari benki hiyo imeanza kufanyia kazi hayo malalamiko baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.

Mwananchi wameandika mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu yoyote lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo >>>“Na sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za kubadilisha haraka”

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa ambapo alitoa mfano wa picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro zitarekebishwa ambapo hivi karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000 kukosewa.

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA TANGANYIKA PAKERS KWENYE MRADI WA NYUMBA ZA NHC

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA  YATEMBELEA   TANGANYIKA PAKERS KWENYE MRADI WA NYUMBA ZA NHC
1Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake na jimbo la Kahama Mbunge Mh. James Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akielekeza jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi. 3Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili Mh. Hery Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli wakimsikililiza 4Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka 5Baadhi ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la NHC. 7Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na shirika hilo la NHC. 8Huu ndiyo uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi mahali ambapo sasa panaanzishwa mradi wa nyumba za NHC. 9Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo. 10Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na mbunge wa Kahama Mh. James Lembeli akishuka kwenye gari katika eneo la Tanganyika Pakers mahali ambapo patatekelezwa mradi wa Kawe City unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC. 12Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu13Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akendelea kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe. 14Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam. 15Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo mikubwa ya makazi , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh.Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo na na Mbunge wa Mafia. 17Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata taarifa ya awali..

WANAO WANIA UONGOZI NDANI YA CHADEMA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA WATWANGANA MAKONDE

hapa ni mahali pa ofisi ya chadema  kwa mkoa wa Shinyanga.

Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,wilaya  ya Kahama mkoani Shinyanga umeingia dosari,baada ya mmoja wa madiwani wa chama hicho kuhusishwa na rushwa na vitendo vya usaliti ndani ya chama kutoka CCM.

MWANAUME APIGWA RISASI TUMBONI NYAKATI ZA MCHANA AKIWA NDANI YA GARI-MAGOMENI DAR

MWANAUME APIGWA RISASI  TUMBONI NYAKATI ZA MCHANA AKIWA NDANI YA GARI-MAGOMENI DAR

Mtu asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.…
Mtu asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.
Muonekano wa nyumba wa gari hilo.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW. Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.
PICHA: HANS MLOLI/GPL

DREVA WA BODABODA AUAWA KIKATILI KISHA MWILI WAKE KUTELEKEZWA KANISANI.

DREVA WA BODABODA  AUAWA KIKATILI KISHA MWILI WAKE KUTELEKEZWA  KANISANI.
Kijana mwendesha pikipiki akibeba abiria maarufu kama (Boda boda) katika manispaa ya Tabora ameuawa na watu wasiojulikana na kumtelekeza aneo la kanisa katholiki Makokola, na kutoweka na pikipiki yake aina ya Sanlg huku kisu kilichodaiwa kutumika kumuua kikitelekezwa eneo hilo.
Akizungumza kwa masikitiko eneo la tukio alipouawa mwendesha pikipiki huyo, katibu wa chama cha waendesha Bodaboda Bw.Kasim Kiduli amesema kuwa, matuikio ya kukatisha maisha ya waendesha pikipiki inaonesha kurudi mkoani Tabora, kwani kulikuwa na ukimya kwa muda.
Baadhi ya wananchi wakiokuwa katika tukio hilo pamoja na kukemea tabia ya mauaji, wamewataka waendesha pikipiki hao kujihadhari na kutofanya kazi nyakati za usiku, kwani katika kubeba unaweza kumbeba adui bila kumjua.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina  msaidizi Suzani Kaganda, amemtaja marehemu kwa jina la Cosmas John, amesema kuwa, pamoja na kifo hicho, katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiojulikana wamewaua mama na watoto wake wawili  wanafunzi wa shule ya msingi Mwamalulu wilayani Nzega.

WATU WATANO WANUSURIKA KUFA KWENYE AJALI YA GARI-KIMARA DAR

WATU WATANO WANUSURIKA KUFA KWENYE AJALI YA GARI-KIMARA DAR
Gari aina ya Mitsubishi Canter likiwa pembezoni mwa barabara baada ya ajali hiyo.
Muonekana wa gari hilo baada ya ajali.

Baadhi ya raia waliokuwa kwenye eneo la tukio
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Watu watano wamenusurika kufa kwa ajali Kimara Dar es Salaam baada ya gari dogo aina ya Toyota Rav 4 iliyokuwa ikitokea Kimara kuelekea Ubungo kuhama upande wa pili wa barabara na kugongana uso kwa uso na gari aina ya Mitsubishi Canter na kusababisha dereva wa Canter kuumia vibaya na kukimbizwa hospitali.
Waliokuwa ndani ya Rav 4 walipata majeraha madogo. Ajali hiyo imetokana na kutereza kwa barabara baada ya mvua kunyesha.
(Habari/Picha na :Global Whatsapp 

MBUNG MREMA ANENA JIMBONI KWAKE AHAMASISHA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Mbunge wa jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa chama cha TLP,Dk.Augustine Lyatonga Mrema akihutubia mkutano wake wa hadhara jimboni kwake  jana kwa ajili ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo,aidha katika jimbo hilo la Vunjo kumekuwepo na Mvutano mkubwa kwa vyama vya CCM,Innocent Shirima na Mh.James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
habari hii kwa msaada wa eddymobilize.blogspot.com
KARENY. Powered by Blogger.