Moja ya mbwa anayedaiwa kumla mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) akiwa ameuawa pia.
MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Ludewa
mkoani Njombe, Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) ameuawa kikatili na mbwa
wanaosadikiwa kuwa na kichaa kisha kuliwa nyama.
Tukio hilo lililoacha simanzi kubwa kwa
wakazi wa Ludewa mjini lilijiri saa 7 mchana wa Agosti 8, mwaka huu
katika eneo la Ikilu ambapo marehemu na wenzake walikuwa wakipita nje ya
nyumba ya mtu aliyejulikana kwa jina la Bosco Lingalangala (Boli)
kwenda kuchuma mapera sehemu.
o.
DAKTARI ALIVYOSEMA
Kwa
mujibu wa taarifa ya Dokta Sira Rajabu wa Hospitali ya Wilaya ya Ludewa
aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Ibrahim, ulikuwa na majeraha
makubwa mwili mzima huku paja la mguu wa kulia likiwa limeondolewa nyama
kabisa.
MGANGA WA MIFUGO
Akizungumza
na paparazi wakati wa msiba wa mtoto huyo, Mganga wa Mifugo wa Wilaya
ya Ludewa, Simon Haule alisema mbwa hao walikuwa hawajapata chanjo kwa
zaidi ya miaka miwili. Kwa hiyo tayari walikuwa na ugonjwa wa kichaa
ambacho kisingeweza kupona tena zaidi ya kuwaua.
Padri akiiombea roho ya mtoto, Ibrahim Faraja Chipungahelo ikapate kupumzika kwa amani.
WANANCHI WAANDAMANA, WAWAUA MBWA
Kufuatia
tukio hilo la kusikitisha, Agosti 10, mwaka huu baadhi ya wananchi wa
Kata ya Ludewa waliandamana ili kushinikiza haki itendeke baada ya
kuambiwa kuwa mmiliki wa mbwa hao alitishia kumshtaki yeyote ambaye
angehusika kuwaua mbwa wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika
mkutano wa dharura ulioitishwa na Diwani Mchilo, wananchi hao walisema
mbwa hao walikuwa tishio kwa muda mrefu kwani walishateketeza mifugo
mingi wakiwemo mbuzi 22 na ndama 1, lakini cha kushangaza kila
walipolipeleka suala hilo kwenye vyombo vya dola, mmiliki alitaka
ushahidi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,
wananchi hao walisitisha mkutano huo na kuandamana mpaka kwenye nyumba
ya mmiliki wa mbwa hao ambapo waliwaua kwa kuwapiga risasi.
MIZOGA MITAANI
Kwa hasira, waliondoka na mizoga na kupita nayo mitaani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kikabila na kawaida.
WACHOMA MOTO MIZOGA
Baada
ya kuzunguka na mizoga ya mbwa hao kwa muda mrefu, mwishowe walikwenda
kwenye ofisi ya kata ambako waliichoma moto na kuiteketeza kabisa huku
wakishangilia.
MKUU WA WILAYA
Kufuatia
tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Juma Madaha ameviagiza vyombo
husika ikiwemo idara ya kilimo na mifugo na jeshi la polisi kuchukuwa
hatua za kisheria kwa yeyote anayehusika na tukio hili akiwemo mmiliki
wa mbwa hao.
Marehemu Ibrahim Faraja Chipungahelo alizikwa Agosti 9, mwaka huu kwenye Makaburi ya Ludewa, Njombe.
Wananchi wakichoma mwili wa mbwa aliyemuua mtoto Ibrahim.
KAMANDA WA POLISI
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Fulgensi Ngonyani alikiri kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea sanjari na
kuwahoji watu mbalimbali, akiwemo mmiliki wa mbwa hao anayeishi jijini
Dar es Salaam.Mungu ailaze pema peponi, roho yake. Amina.