Habari za hivi Punde

MAGARI HAYA MAKUBWA YAMEKUWA YAKIEGESHWA KANDOKANDO YA BARABARA KUU IENDAYO MWANZA MAJIRA YA KUANZIA SAA MOJA JIONI NA KUHATARISHA USALAMA BARABARANI MJINI SHINYANGA




NJIA YA KUTUMIA SHANGA IMEELEZWA NI BORA ,UZAZI WA MPANGO UNATAKIWA KATIKA JAMII.


Shanga iliyoshikwa mkononi na  mtoa huduma ya afya ya uzazi ambayo imebuniwa na wizara ya afya  kwa lengo la kuwasaidia wanafamilia kupanga uzazi kwa kutumia njia hiyo ambayo imeonekana ni rahisi ,ikiwa njia zote mtu anauhuru wa kuchagua.hivyo jamii imetakiwa kuondoa dhana potofu dhidi ya utumiaji wa njia zilizopo kuwa zina madhara huku wakiziacha na kutumia njia ambazo sio salama.



Hili ni moja wapo la banda lililo kuwa likitoa huduma ya uzazi wa mpango katika  uwanja wa shy-com.
  
 
Wa kwanza kushoto ni Mkuu  wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa na mganga mkuu wa mkoa  Ntuli Kapologwe pamoja na mkuu wa wilaya  ya Shinyanga bi Annarose  Nyamubi wakati wakijiandaa kwenda kukagua mabanda ya watoa huduma za afya ikiwemo uzazi wa mpango ambapo mkuu wa mkoa alizindua  mpango huo huku akiwataka wananchi mkoani humo kutumia njia ya uzazi wa mpango ili kuweza kuleta uiano bora katika malezi ya watoto na kupata mafanikio.


MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ALLY RUFUNGA AKIWA KATIKA VIWANJA VYA SHY-COM AKITEMBELEA MABANDA YA WADAU WA AFYA MKOANI HUMO.



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga  akiwa na mganga mkuu wa mkoa  Ntuli Kapologwe katika viwanja vya shy-com mara baada ya kuwa amewasili katika uzinduzi wa  mpango wa uzazi huku kauli mbiu fuata nyota ya kijana ili upate mafanikio.


Mkuu wa mkoa  wa Shinyanga akiwasili katika banda la redcross kwa lengo la kupata maelezo namna wanavyo hamasisha jamii ili waweze kutoa damu.


Wadau wa afya wakijiandaa kutoa maelezo baada ya kumuona mkuu wa mkoa karibu yao ambaye hayupo pichani kwa lengo la kutoa maelezo namna wanavyo wajibika.


WADAU WA AFYA KATIKA MKOA WA SHINYANGA WAKIWA KATIKA MABANDA YAO WAKIHAMASISHA UZAZI WA MPANGO NA UPIMAJI WA VVU.


Add caption



RED CROSS IKIHAMASISHA UTOAJI WA DAMU SALAMA KWA WANANCHI BAADHI WAJITOKEZA.


Kijana akitoa damu katika banda la red cross  katika uhamasishaji wa damu salama kwenye kampeni ya uzinduzi wa uzazi wa mpango uliozinduliwa na mkuu wa mkoa  huku wadau mbalimbali wa afya wakijitokeza kwa huduma mbalimbali


Maandamano yaliyofanywa na idara ya afya kwaajili ya uhamasishaji wa  uzazi wa mpango  mara baada ya kuzinduliwa katika mkoa wa Shinyanga.


Kijana huyu akiwa pembeni na mtaalamu kutoka red cross baada ya kupata ushauri akisubiri kutoa damu.


DKT ROSE AKIELEZEA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZOTE NI SALAMA NA HAZINA MADHARA BALI KILA MMOJA ANAUHURU WA KUTUMIA NJIA AIPENDAYO.


Dkt Rose Madinda  ambaye ni mshauri wa masuala ya afya  akielezea changamoto za wanawake kuhusiana na  utumiaji wa njia ya uzazi wa mpango ambapo anasema  njia hizo  ni salala hazina madhara yoyote kama inavyoelezwa huku akiwataka kuacha kutumia  njia ambazo sio za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti na badala yake kutumia njia potofu ni kuongeza madhara zaidi katika mwili.


WADAU WA AFYA MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA TAARIFA KUHUSIANA NA UZAZI WA MPANGO KATIKA JAMII AMBAPO MKOA WA SHINYANGA UMEFIKIA ASILIMIA 12.5 KWA WANAOTUMIA NJIA YA UZAZI WA MPANGO.


Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli  Kapologwe akielezea wadau wa masuala ya afya mkoani humo jinsi ya mikakati ya uhamasishaji  wa uzazi wa mpango katika jamii ambapo kimkoa umekuwa  na asilimia 12.5 ya idadi ya watu wanao tumia uzazi wa mpango kwa njia ya kisasa.



Wadau wa afya mkoani Shinyanga  wakisikiliza taarifa iliyotolewa  dhidi ya  wizara ya afya huku wakilalamika  kuhusiana na takwimu zinazotolewa ,ambapo wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii  jinsi ya utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango ikiwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakilalamika na kudai kuwa  njia hizo zimekuwa zikiwaletea madhara  ikiwa wataalamu hao wamesema sio kweli ni njia bora  na kila mmoja ana uhuru wa kuchagua anayoipenda.


Wadau wa afya mkoani Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa mkuu wa mkoa ambapo wakijadiliana  suala la uzazi wa mpango huku aliyesimama ni Dkt Gregory  Kamugisha kutoka chuo kikuu cha John Hopkins kilichopo nchini Marekani kwa tawi la Dar-es-salaam huku akieleza kuwa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango kwa mkoa wa Shinyanga upo chini ambapo imeelezwa kuwa  wanawake waishio vijijini kwa wastani  ni asilimia 6.1 huku mijini ni asilimia 3.7 ya wanawake wenye watoto kwa tawkimu zilizotolewa na wizara ya afya mwaka 2010.


WANAFUNZI NA WALIMU SHULE YA MASAGALA WAPATIWA ELIMU NA IDARA YA UHAMIAJI.


Baadhi ya walimu wa shule ya msingi Masigala wakipatiwa elimu na afisa  kutoka idara ya uhamiaji mkoa ambaye hayupo pichani.


Shule ya msingi Masagala  ambayo imejiwekea jukumu la kuwa na kisima cha kuhifadhi maji kwaajili ya kumwagilizia  bustani za maua shuleni hapo na kufanya shule kuwa miongoni mwa shule zinazotunza mazingira.


Wanafunzi wa shule ya msingi Masagala iliyopo kata ya  Songwa wilayani Kishapu wakipatiwa elimu  na  ofisa wa uhamiaji mkoa wa Shinyanga ambaye hayupo pichani.


MAANDAMANO YALIYOFANYWA NA WANAWAKE WA UWT MANISPAA YA SHINYANGA LENGO KUPINGA UKATILI WA WATOTO.


BAADHI ya wakazi wa manispaa ya Shinyanga wakifanya maandamano ya kupinga  ukatili dhidi ya watoto ambayo yamekuwa yakifanywa na  baadhi ya waendesha daladala za baiskeli  kwa kuwafanyia watoto vitendo vya ubakaji huku wakiaachia ulemavu kwa kuwatoboa macho.


Wakazi hao waliokusanyana katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini  waliamua kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kutaka waendesha dalala hao wawe na usajili  maalumu wa kuwatambua au kuondoka kabisa na kuwepo kwa usafiri wa daladala za magari kama wafanyavyo  mikoa mingine.


Zoezi la maandamano  lilianza huku wakiimba nyimbo za kupinga ukatili wa watoto ambapo maandamano hayo yalipokelewa   na mkuu wa wilaya Annarose Nyamubi yalipofika ofisini kwake sanjari na mbunge viti maalumu Azzah  Hillali akiomba serikali kuangalia suala hilo ili kuweza kunusuru watoto ambao ni taifa la kesho.


KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA SHINYANGA KIKIPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA HICHO.


Katibu wa CCM katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini   akijitambulisha kwa mara ya kwanza  kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya hiyo mara baada ya kuwa amehamia akitokea mkoani Kagera.


Katibu wa CCM  mkoa wa Shinyanga Adam Ngalawa  akimpa mkono mzee Masale Sengerema wakati alipoteuliwa na mwenyekiti wa wilaya ya Shinyanga  Mwenzetu Mgeja  kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya  CCM wilaya.



Mkuu wa wilaya  ya Shinyanga Annarose Nyamubi  akisoma taarifa ya utekelezaji  ya ilani ya chama hicho mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Shinyanga vijijini.


HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA KUJENGWA KIJIJI CHA NEGEZI KATA YA MWAWAZA MANISPAA YA SHINYANGA.


wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wakifutilia kwa ukaribu ujenzi unaoanza kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa  ambapo ziara hiyo iliongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga
ambapo ujenzi huo unajengwa katika eneo la kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga akiwa kwenye eneo linalojengwa hospitali ya rufaa ya mkoa  akimueleza mwenyekiti wa CCM mkoa Khamis Mgeja ambapo ujenzi huo utagharimu  kiasi cha shilingi  billioni  89.6.


Baadhi ya mafundi wakiwa kwenye eneo la ujenzi huo ambapo wameanza kuchimba msingi.


Wajumbe hao wakiangalia eneo hilo na jinsi ya ujenzi unavyokwenda ambapo inaelezwa kuwa  pindi itakapo kamilika hospitali hiyo itaweza kuondoa msongamano wa wagonjwa  katika hospitali ya mkoa  ikiwemo wagonjwa kusafirishwa au kusafiri umbali mrefu kwa lengo la kutafuta matibabu.


ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI KATA YA TINDE KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA


Mbunge viti maalumu Azzah Hillai akimueleza naibu waziri wa maji Amosi Makala  uhaba wa maji safi na salama katika kata ya Tinde  ambapo waziri huyo alitembelea miundombinu mbalimbali ya maji ili kujionea hali halisi.
Ikiwa baadhi ya wananchi walimuletea maji wanayotumia kwa kunywa  kama hapo  yanavyoonekana meza kuu kwenye jagi na chupa.


Baadhi ya vijana wakiwa na mkokoteni  unaokokotwa na punda  utakao beba madumu ya maji kwa lengo la kuyapeleka mjini  na kufanya biashara ikiwa dumu moja ni shilingi 300 hadi 400.


Naibu waziri wa maji akionyesha  bwawa la jomu lililopo kata ya Tinde ambalo hutegemea maji yake kwa kunywa  na dumu moja huuza shilingi 200 kwa maji yanayotoka kwenye mto huo,huku diwani wa kata hiyo Jafari Kanoro akieleza kuwa maji hayo yamekuwa yakisaidia ila kinachotakiwa uongozi wa wizara na halmashauri ulione suala hilo la kusafisha magugu maji hayo ndiyo imekuwa kilio chao kikubwa.


Naibu waziri akiwa katika mkutano wa hadhara,baadhi ya wananchi walimpelekea maji ili naye anywe ikiwa alinyanyua chupa moja ya maji na kuwaonyesha kuwa anao uwezo wa kunywa maji hayo ila kinacho takiwa ni kupatikana kwa maji safi  na salama ya kunywa
Ambapo aliwaahidi   muda sio mrefu watapata maji hayo,huku akiwataka wataalamu kutoka wizarani kushughulikia suala hilo ndani ya siku 14  huku akiwataka wananchi pindi watakapo kuja kufanya utafiti wapewe ushirikiano na kusiwepo mgogoro wa aina yoyote hivyo wizara itahakikisha mashine ya kuchimba kisima kirefu inakuja Tinde na kazi inaanza mara moja.


BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI WAKITOA MALALAMIKO YAO DHIDI YA MIFUKO YA HIFADHI.


Mwenyekiti  wa chama cha watumishi wa serikali za mitaa TALGHU tawi la Shinyanga  Christopher Malengo alipokuwa akiwasilisha malalamiko dhidhi ya mifuko ya hifadhi kuwa imejikita kusaidia wafanyakazi  na kutumia  fedha hizo kwaajili ya uwekezaji ,ikiwa alishauri kuwa  wenye mifuko hiyo watengeneze utaratibu wa kuwekeza kwa kukopa wafanyakazi  pindi bado wawapo kazini kuliko kusubiri uzeeni,
Hata hivyo aliwaeleza mamlaka ya mifuko ya hifadhi  SSRA  kuwa mwajiri anachangia asilimia 15,  mwajiriwa asilimia 5,na kuchukua baada ya miaka zaidi ya 20  sasa kwanini usiwepo utaratibu pia wa  hao wenye mifuko kuchangia nao asilimia mbili.


Baadhi ya  viongozi wa  vyama vya wafanyakazi wakiwa katika moja ya semina iliyoandaliwa na mamlaka ya mifuko ya jamii nchini  SSRA ,ambapo walieleza kuwa kwanini usiwepo mfuko mmoja wenye kuleta mlingano wa mafao kuliko hivi sasa kumekuwepo na ubabaishaji mwenye miaka michache kazini kulipwa zaidi kuliko aliyefanya miaka mingi,huku baadhi ya mifuko imekuwa haitoi  maelezo kwa wateja wao.


BAADHI YA ASKARI MKOANI SHINYANGA WAKIPATIWA SEMINA FUPI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII (SSRA)

Baadhi ya Askari  mkoani Shinyanga wakisikiliza moja ya semina iliyoandaliwa na mwamvuli wa mifuko ya jamii nchini SSRA ambapo semina hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa Ibanza hotel  huku wakiwa na  shauku kubwa ya kujua  changamoto zinazowakabili baada ya kujiunga na mifuko ya hifadhi mbalimbali.

Insp  Robert Mageta  wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga  akiuliza swali juu ya mafao wanayokatwa  katika mifuko mbalimbali  huku akieleza  baadhi ya miaka wanayokatwa  mafao hayaonekani.

WP  Rose   akitoa  ushauri kwenye mamlaka ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa  ni bora kungekuwepo na mfuko mmoja wenye kueleweka na kutoa mafao sawa kuliko ilivyo mingi na kuonekana kuna ubabaishaji ndani yake.

Baadhi ya askari wakiwa katika picha ya pamoja na  wakufunzi mara baada ya kumaliza semina  hiyo.

JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LIKIPATIWA SEMINA JUU YA MIFUKO YA HIFADHI.


Mwanasheria  mwandamizi wa SSRA kutoka jijini Dar-es-salaam Salma Maghimbi akitoa elimu juu ya mifuko ya hifadhi nchini inavyofanya kazi  katika  semina iliyowahusisha  jeshi la polisi mkoani Shinyanga  huku nao wakieleza changamoto wanazokumbana nazo  mara walipojiunga kwenye mifuko hiyo.


ALBINO AUWAWA KIKATILI WILAYANI BARIADI

ALBINO AUWAWA KIKATILI WILAYANI BARIADI
Bariadi. Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) yamezuka upya mkoani Simyu, ambapo mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) ameuawa kinyama kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana pamoja na kutoweka na baadhi ya viungo vyake.
 
Tukio hilo lililotokea katika kitongoji cha chalala kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani Bariadi Mkoani hapa, marehemu alikatwa mguu wake wa kushoto sehemu ya goti, vidole 2 mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba , ambapo wahusika walitoweka na viungo hivyo.

SSRA YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA.


Wajasiliamali manispaa ya Shinyanga wakipatiwa elimu juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii inavyonufaisha maisha ya baadaye hivyo ni muhimu kujiunga kwao


WATOTO NA AKINA MAMA WAANDAMANA KUPINGA UKATILI UNAOFANYWA NA KIKUNDI CHA BOKO HARAMU

WATOTO NA AKINA MAMA WAANDAMANA KUPINGA  UKATILI UNAOFANYWA NA KIKUNDI CHA BOKO HARAMU

WATOTO na akina mama  manispaa ya Shinyanga  wameandamana  kwa lengo la kupinga ukatili dhidi ya watoto wa kike uliofanywa  na  kundi la waharamia  wa kiislamu linalojulikana  kama boko  haramu  lililopo  nchini Nigeria  mara baada ya  kuwateka wanafunzi  zaidi ya 270.

Maandamano hayo  yalishirikisha pia  shirika  lisilo la kiserikali la AMSK FOUNDATION la mjini Shinyanga linalojihusisha na shughuli za kutetea ukatili dhidi ya watoto wa kike na akina mama  huku mkurugenzi  mtendaji wa shirika hilo Lilian Kowfie akieleza kuwa  wameamua kufanya hivyo ili kukemea vitendo viovu vinavyofanywa kwa watoto wa kike.

WAJASILIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA WAPATIWA ELIMU YA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI.

WAJASILIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA WAPATIWA ELIMU YA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI.
WAJASILIAMALI  manispaa ya Shinyanga  wamepatiwa elimu  juu ya kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ili kuweza kuboresha maisha yao na kuondoa dhana ya  mifuko hiyo  kuwa inawahusu waliopo kwenye sekta rasmi pekee kama ilivyo kuwa awali.

 Kwa sasa  mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) imeamua kutoa fursa hata kwa wajasiliamali  wanaofanya biashara ndogondogo kujiunga na mifuko hiyo   kwa mujibu wa Hifadhi ya mifuko ya jamii ni haki ya kila mtu kujiunga nayo, haki hii imeanishwa katika ibara  ya 11 (1) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003.

MAMLAKA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YATAKIWA KUSIMAMI ILI KUONDOA UTAPELI UNAOFANYWA.

MAMLAKA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YATAKIWA KUSIMAMI ILI KUONDOA UTAPELI UNAOFANYWA.
BAADHI ya wajiriwa  katika sekta mbalimbali mkoani Shinyanga  wameitaka  mamlaka ya mfuko wa hifadhi ya jamii nchini  (SSRA)  kuzisimamia hifadhi zilizopo ili kuacha kufanya kazi kwa kutapeli  bila kueleza  viwango vya fedha  wanavyokusanya hali ambayo imejidhihirishia hata kipindi cha kustaafu kupokea mafao yao kidogo tofauti na wanavyotarajia.

Hata hivyo imebainika kuwa watumishi wapya wa serikali hususani waajiriwa wapya kutoa fomu ambazo zimeshajazwa bila kutoa ushauri  mzuri, hali ambayo inasababisha baada ya muda wateja wao kujutia kujiunga na baadhi ya  mifuko hiyo.

ZAIDI YA WAKULIMA 14,000 WAMEBAINIKA KUPATA HASARA KWA KUTUMIA MBEGU ZISIZO NA MANYOYA NA KUTOOTA. VIZURI

ZAIDI YA WAKULIMA 14,000 WAMEBAINIKA  KUPATA HASARA KWA KUTUMIA MBEGU ZISIZO NA MANYOYA NA KUTOOTA. VIZURI



IMEBAINIKA kuwa  wakulima wa zao la pamba  zaidi ya 14,000 nchini wamepata hasara baada ya kupanda ekari 50 elfu kwa kutumia  mbegu zisizo na manyoya za Quiton na kushindwa kuota, huku wilaya ya Kishapu ikiwa ni miongoni  kwa kupata hasara ya billion 1.6 ambazo zingetokana na kuuza zao hilo.

Katika mikoa sita na wilaya 23 ,ambapo ekari 50 ,000 hazikuota  zilizopandwa kwa kutumia mbegu ya quiton UK 91 na UK 08 ,ambazo zilifanyiwa utafiti katika chuo cha Ukiriguru jijini Mwanza na kuonekana zinafaa kwa kuwa na ubora mkubwa utakaosaidia kuongeza uzalishaji

MRADI WA BWAWA LA ISHOLOLO WAMSIKITISHA NAIBU WAZIRI WA CHAKULA KILIMO NA USHIRIKA ALIPOPATIWA MAELEZO JUU YA KUKWAMA KWAKE

MRADI WA BWAWA LA ISHOLOLO WAMSIKITISHA NAIBU WAZIRI WA CHAKULA KILIMO NA USHIRIKA ALIPOPATIWA MAELEZO JUU YA KUKWAMA KWAKE

MRADI  wa  mbwawa la umwagiliaji  katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule halmashauri ya  wilaya  Shinyanga  umeingia  sura mpya mara baada ya naibu waziri  wa kilimo,chakula  na ushirika  Godfrey  Zambi  kuutembelea  na kujionea  hali halisi  ya kutokamilika  kwake ingawa  mkandarasi  ameongezewa muda  huku akisikitishwa na  uongozi ngazi ya kanda,mkoa  na wilaya kutoshirikishwa na kuutambua.

“Nina kiri  baadhi ya miradi  imetumia fedha nyingi zaidi ya shilingi  million 200 lakini miradi hiyo imefanywa vibaya ,pia serikali  ilidhamiria  kuweka mradi huu hapa  hali imeonekana mkandarasi  ndio hovyo na kutokuwa na uwazi  kwenye mradi,  ikiwa uongozi wa ngazi mbalimbali unaotegemewa haujashirikishwa.”alisema Zambi.

MRADI WA MBWAWA KATIKA KIJIJI CHA ISHOLOLO WILAYANI SHINYANGA WASHINDWA KUKAMILIKA.


Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi  akiwa katika mradi  wa bwawa la Ishololo katika kijiji hicho kata ya Usule wilayani Shinyanga sambamba na mbunge viti maalum Azzah Hillali ambapo mradi huo umeshindwa kuisha ingawa umetumia kiasi cha shilingi millioni 940 huku mkandarasi wake akidaiwa kukosa vifaa na kuendeleza shughuli zake binafsi.


HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU IKITOA TAARIFA YA MIRADI YA UMWAGILIAJI.


ugeni wa naibu waziri  wa kilimo,chakula na uchirika Godfrey Zambi akiwa  ameambatana na  injinia wa kanda  ya ziwa Ebenezer Kombe  sanjari na mkuu wa wilaya ya Kishapu  mkoani Shinyanga Wilson Nkhambaku katika ukumbi wa halmashauri  lengo kupata taarifa za  awali kuhusu miradi ya umwagiliaji.


NAIBU WAZIRI WA KILIMO ,CHAKULA NA USHIRIKA AKIKAGUA MRADI WA BANIO KATIKA KIJIJI CHA ITILIMA WILAYANI KISHAPU.


Naibu waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi  akikagua  mradi wa banio kwaajili ya umwagiliaji  ambao haufanyi kazi licha ya kutumia gharama kubwa kwa ujenzi  huku akisikitishwa na uotaji nyasi   na kufanya kukosekana kwa njia  ya kuelekea kwenye banio hilo.


MRADI WA BANIO KWAAJILI YA UMWAGILIAJI HAUJANUFAISHA WAKULIMA WA KIJIJI CHA ITILIMA


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku  akisoma taarifa  ya awali  ya ukaguzi wa mradi wa  banio la umwagiliaji lililopo katika kijiji cha Itilima wilayani humo ambalo limetumia kiasi cha shilingi millioni  302.1 mpaka sasa halifanyi kazi.

KARENY. Powered by Blogger.